Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MWAMKO mdogo wa wajasiriamali katika kujitokeza kwenye mafunzo yanayotolewa bure, umetajwa kuwa chanzo kikubwa cha kushindwa kupamabana na umasikini.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (Sido) mkoani hapa, Abel Mapunda wakati akizungumza na Tanzania Daima.
Alisema wajasiriamali walio wengi wako tayari kuendesha biashara zao bila utaalamu zaidi, jambo linalowafanya kutolipa kipaumbele mafunzo.
“Walio wengi wakielezwa kuwa kuna mafunzo juu ya ujasiriamali wanaoufanya, hawako tayari hata kama mafunzo hayo yanatolewa bure,” alisema.
Mapunda alisema kutokana na umuhimu huo, aliwataka wajasiriamali hao kulipa kipaumbele suala la mafunzo ili waweze kuboresha utengenezaji wa bidhaa zao na namna ya kupata masoko kwa wakati.
Pia alisema kwa sasa Sido inaendesha mafunzo kwa vijana wapatao 35 ambao wanafundishwa kutengeneza bidhaa za ngozi baada ya kuingia mkataba na Shirika la Misaada la Uholanzi.
Alisema mafunzo hayo yalianza Oktoba mwaka huu, na yatafungwa Novemba mwaka huu, ambapo kati ya washiriki 35, washiriki 10 ni wanawake na 25 ni wanaume.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment