Mbunge wa Bahi, Dodoma, Omary Badwel (CCM).
Ameiomba mahakama imetendee haki kwa madai ya kwamba tuhuma dhidi yake zilikuwa njama za kuchafua jina lake.
Badwel alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa, alipokuwa akitoa utetezi wake.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Badwel anadaiwa kati ya Mei 30 na
Juni 2, 2012, katika maeneo tofauti mkoani Dar es Salaam, alishawishi
apewe rushwa ya Sh. milioni nane kutoka kwa Sipora.
Inadaiwa Badwel aliomba rushwa hiyo ili ashawishi wajumbe wengine
wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), kupitisha
hesabu za halmashauri hiyo.
Pia anadaiwa Juni 2, 2012 katika hoteli moja iliyoko wilayani Ilala, alipokea rushwa ya Sh. milioni moja kutoka kwa Sipora.
Akiongozwa na Wakili wa utetezi Mpare Mpoki, Badwel, alidai hajawahi kuomba rushwa wala kuwa na nia hiyo.
“Sijawahi kupokea rushwa ya kiasi hicho kutoka kwa Sipora. na wala
sijawahi kumshawishi na katika maelezo yake Sipora aliyoyatoa mahakamani
amekiri sijawahi kumuomba rushwa,” alidai Badwel
Alidai katika kamati hiyo kuna wabunge 15 na yeye ni mmoja wa
wajumbe, hivyo asingeweza kuwashawishi kwa sababu hakuwa na mamlaka
hayo.
Alidai jukumu moja wapo la kamati hiyo ni kupokea taarifa za
ukaguzi wa fedha kutoka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG), ambapo inazipitia na kuwaita mkurugenzi na wakuu wa idara za
halmashauri husika na kuwasomea taarifa na kutoa ushauri.
Alidai lengo ni utaratibu wa uwajibikaji wa watu kufanya kazi na
kukaguliwa na kutolewa taarifa na iwapo halmashauri zimefanya vizuri
wanaishauri serikali kuzipongeza na ikiwa hazijafanya vizuri zichukuliwe
hatua.
Alidai taarifa ambayo imeshakaguliwa na CAG, kamati ya Bunge haina uwezo wa kuibadilisha kwa namna yoyote.
CHANZO:
NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment