Home » » MKUTANO WA ISHIRINI WA BUNGE LA KUMI KUANZA DODOMA TAHERE 12 MEI 2015

MKUTANO WA ISHIRINI WA BUNGE LA KUMI KUANZA DODOMA TAHERE 12 MEI 2015

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA



1.0       UTANGULIZI
Mkutano wa Ishirini (20) wa Bunge la Kumi (10) unatarajia kuanza mjini Dodoma tarehe 12 Mei 2015. Mkutano huo ambao ni mahususi kwa ajili ya kujadili na kupitisha Bajeti ya Serikali ndiyo utakaokuwa mkutano wa mwisho wa Bunge hili kabla ya kuvunjwa na baadaye kufanyika Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2015.

Hivyo, Wabunge wote wanapaswa kuwa wamewasili mjini Dodoma  ifikapo Jumapili tarehe 10 Mei 2015 tayari kuhudhuria kikao cha briefing siku  ya Jumatatu tarehe 11 Mei, 2015.

2.0       SHUGHULI ZITAKAZOTEKELEZWA
Katika Mkutano huu kutakuwa na wastani wa maswali 295 ya msingi yatakayoulizwa na kupatiwa majibu. Aidha, kutakuwa na wastani wa maswali 56 atayoulizwa Waziri Mkuu na kuyapatia majibu kwa mujibu wa Kanuni ya 38(1) ya  Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Aprili 2013.

Aidha, katika mkutano huo, taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2013/2014 itawekwa mezani na kufuatiwa na taarifa yenye majibu kuhusu hoja zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Hesabu za mwaka wa Fedha wa 2013/2014.

Baada ya hayo, Bunge litapokea na kujadili utekelezaji wa Wizara zote 24 wa Bajeti kwa mwaka wa Fedha unaoisha pamoja na Makadirio na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016.

Siku ya Alhamisi tarehe 11/Juni/2015 saa 4:00 (nne)  asubuhi Waziri anayehusika na Mipango atawasilisha taarifa ya Hali ya Uchumi wa Nchi, ikifuatiwa na hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016 itakayosomwa na Waziri wa Fedha saa 10:00 jioni. Wabunge wote mnaombwa kuwepo Dodoma.

Mjadala wa hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha wa 2015/2016 utaanza na utafuatiwa na kupitishwa kwa Muswada wa Sheria ya Matumizi wa Mwaka 2015 pamoja na kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria wa Fedha wa Mwaka 2015.

3.0 SHUGHULI NYINGINE
Shughuli za Mkutano wa 20 zinatarajiwa kumalizika tarehe 27 Juni, 2015 na kuhitimishwa kwa hotuba ya Waziri Mkuu ya kuliahirisha Bunge.

Ratiba kamili ya shughuli za Mkutano wa Ishirini wa Bunge la Kumi itapatikana kwenye Tovuti ya Bunge ambayo ni www.parliament.go.tz


Imetolewa na:
Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,
DAR ES SALAAM
08  Mei 2015




0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa