Home » » VIKAO VYA KAMATI MBALIMBALI CCM VYAANZA LEO,,MGOMBEA WA URAIS KUPATIKANA KWA MFUMO WA 38-5-3-1...‏

VIKAO VYA KAMATI MBALIMBALI CCM VYAANZA LEO,,MGOMBEA WA URAIS KUPATIKANA KWA MFUMO WA 38-5-3-1...‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Ilianza miaka ikaja miezi na sasa ni saa 144 zilizobaki ili kumpata mgombea kuwania nafasi ya rais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
Ni ukweli usiyopingika kuwa masaa hayo 144 yanawatia matumbo joto wagombea 38 waliomba ridhaa ya kuteuliwa katoka chama cha mapinduzi CCM  huku mkoa wa Dodoma ukifurika wageni mbalimbali na wana CCM watakaohusika katika mchakato wa kumpata mgombea atakaesimamishwa na chama kupitia mkutano mkuu.
Wagombea hao ambao walichukuwa fomu za kwania nafasi hiyo na kufanya idadi ya watangaza nia kufikia 42 wapo pia ambao kwa sababu mbalimbali walishindwa kufika kileleni hivyo kubaki waombaji 38 ambao sasa rasmi wanaingia kwenye mchakato wa mchujo kwa mtindo wa 38-5-3-1.
Tangu kuanza kwa mchakato huo Juni 3 mwaka huu wagombea wote 42 walitimiza masharti yote ya uchukuwaji wa fomu ambapo wagombea 4 walishindwa kurudisha fomu kwakutoa sababu mbalimbali.
Mapema leo akitoa ratiba ya vikao Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye  amesema Julai saba mwaka huu kutakuwa na mkutano wa sekretarieti ya halmashauri kuu ya Taifa CCM ikiwa chini ya Abdulrahman Kinana ambayo agenda yake kuu ni kupitia maandalizi ya vikao vitakavyoendelea baada ya leo Julai 07,2015.
Julai 8  mwaka huu kutakuwa na kikao cha usalama na maadili ya Chama hicho chini ya Mwenyekiti wa chama Taifa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na Julai 9 ni uziduzi wa ukumbi mpya wa CCM na ofisi zake uliopo makulu manispaa ya Dodoma na baada ya hapo mchana kutakuwa na kikao cha kamati kuu ya halmashauri kuu ya Taifa ya CCM.
Lakini pia Julai 10 kutakuwa na kikao cha kamati kuu ya Halmashauri kuu ya taifa ambapo kikao hicho kitateua  jina la MGOMBEA  urais wa Nzanzibar, kupitia ilani ya uchaguzi ya chama hicho itakayotumika kuombea kura na halmashauri hiyo kuu pia itapokea majina matano kutoka kamati kuu ambayo yatapigiwa kura na kubaki majina matatu.
Vunja jungu itakuwa ni Julai 11 ambapo kutakuwa na mkutano mkuu wa Taifa  CCM, mkutano huo utakuwa na kazi kuu mbili ambazo ni; kupitia ilani ya chama na kupiga kura kwa majina matatu yatayokuwa yamewasilishwa kwenye mkutano huo ili kupata jina moja la mgombea atakaeiwasilisha CCM katika kinyang'anyiro cha urais.
Hakika huo ndiyo mfumo rasmi wa CCM katika mchakato wa kumpata mgombea hivyo ukiangalia mfumo ni dhahiri tutakubaliana kwamba katika safari hiyo ndefu tukianza na ile ya awali ya kutangaza nia na baadae uchukuaji na urudishaji fomu mwisho wake tunapata jibu moja tu kwamba ndani ya uwanja wa kuwania kugombea urais kupitia CCM mfumo ni 38-5-3-1. 
Hivyo maana yake ni kwamba mchujo utapita kutoka waombaji 38 hadi 5 na kutoka 5 pia watachujwa na kubaki 3 na mwisho katika hao watatu ni lazima apatikane mmoja hiyo ndiyo maana halisi ya mfumo wa 38-5-3-1.
Masikio, macho na minong'ono ya watanzania ni juu ya nani atasimamishwa na chama hicho lakini mpaka sasa hakuna mwenye jibu iwe ndani ya chama ama nje ya chama, mwisho wa siku tunasubiri matokeo ya mkutano mkuu ambao bila shaka utakuja na jina lenye faraja kwa watanzania.
Kila la kheri Chama cha Mapinduzi......

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa