Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Dodoma.
Migogoro
ya ardhi wanayokabiliana nayo wakazi wa Kata ya Dodoma – Makulu, kwenye
Manispaa ya Dodoma, imeelezwa kuwa itatumika kama kigezo
kitakachotumiwa na wakazi hao, kuchagua viongozi katika ngazi za
udiwani, ubunge na urais, unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Hayo yalielezwa na baadhi ya wakazi wa Mitaa ya Kisasa, Medeli na
Bwawani, wakiwa kwenye ofisi za CCM za Kata ya Dodoma Makulu
walipomsindikiza mtia nia ya kuwakilisha chama hicho katika uchaguzi wa
diwani wa kata hiyo, Lazaro Chihoma, aliporejesha fomu.
“Wakazi wa mitaa karibu yote ya kata hii, tumekubaliana Chifu wetu
(Chihoma) awe kiongozi wa kisiasa wa kata yetu, kwa sababu kwa muda
mfupi ambao amekuwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Bwawani, ametetea
haki zetu dhidi ya waliotudhulumu ardhi,” Mchungaji wa Kanisa la Mitume,
Yohana Mabene, alieleza.
Naye George Michael, mkazi wa Mtaa wa Medeli, alisema mtaa huo
hauna mwenyekiti kufuatia wananchi kugoma katika uchaguzi wa viongozi wa
serikali za mitaa nchini, kutokana na aliyekuwa mwenyekiti kwa zaidi ya
miaka kumi, Stanley Chibwete, kudaiwa kuwa mgombea pekee aliyetakiwa
kupigiwa kura.
Naye Chiloma ambaye pia ni chifu wa watu wa kabila la Kigogo,
akizungumza mara baada ya kuwasilisha fomu za kuwania udiwani wa kata
hiyo ambayo kwa sasa inaongozwa na diwani wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), alisema ameridhia ombi la wananchi wa kata hiyo na
aliahidi kuwatumikia bila kuwaangusha.
Alisema endapo atachaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo, ataendelea
kutumia njia ya mazungumzo na maafikiano, kati yake kwa niaba ya
wananchi anaowaongoza pamoja na mamlaka zinazohusika na usimamizi wa
matumizi ya ardhi, kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake
anayostahili.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment