Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
BUNGE
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mradi wake wa kuwajengea
Uwezo Wabunge na Watumishi (LSP) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo
la Umoja wa Mataifa UNDP kwa mara ya Pili mwaka huu limeratibu Bunge la
Vijana kwa kushirikisha Wanafunzi zaidi ya 100 kutoka Taasisi za Elimu
ya Juu hapa Nchi ambao ni viongozi katika Serikali zao. Bunge hilo
ambalo limeanza Jumamosi tarehe 15 Julai, 2015 na linatarajiwa
kumalizika tarehe 19 Julai 2015.
Spika wa Bunge la Vijana kwa mwaka 2015 Baraka Thomas (UDSM) akiongoza vikao vya Bunge
Waziri
Mkuu katika Bunge la Vijana kwa mwaka 2015 Alexandra Wasonga (ARDHI)
akijibu Maswali ya papo kwa papo Bunge wakati wa Kipindi cha Masuali kwa
Waziri Mkuu.
Mwanasheria
Mkuu katika Bunge la Vijana kwa mwaka 2015 Gama Zulu Leonidas (SAUT)
akiwasilisha Muswada wa Serikali wa Kuanzisha sheria ya Baraza la Vijana
la Taifa wa Mwaka 2015 Bungeni jana.
Wajumbe wa Bunge la Vijana wakishiriki Vikao vya Bunge hilo Mjini
Dodoma.
Bakari Ibrahim (MKWAWA) akiwasilisha Mchango wake kuhusu Muswada huo Bungeni.
Mbunge
wa Bunge la Vijana Shughaib Abdi (CBE) akielezea baadhi ya mapungufu
yaliyopo katika Muswada huo wakati wa Mjadala wa kujadili Muswada huo
Bunging.
Daudi Maneno (MUST) nae akitoa dukuduku lake wakati wa Majadiliano Bungeni.
Waziri
kivuli wa Vijana kutoka Kambi Pinzani kwenye Bunge la Vijana Bi. Joyce
Shirima akielezea baadhi ya Mapendekezo ambayo yanastahili kuingizwa
kwenye Muswada wakati wa Majadiliano Bungeni.
Afred
Salwa (MZUMBE) akiwasilisha Mchango wake kuhusu Muswada wa Baraza la
Vijana la Taifa wa Mwaka 2015 wakati wa kipindi cha majadiliano kwenye
Bunge hilo
Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.
0 comments:
Post a Comment