Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akitoa hotuba ya kuhitimisha
Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa kwenye
viwanja vya Nane Nane Nzuguni Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.Picha na John Banda wa Pamoja Blog.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akimkabidhi zawadi Mwanafunzi
Margreth Mussa wa shule ya msingi Maria de Matias baada ya kushinda
shindano la kuandika insha ya lishe na unyonyeshaji wakati wa sherehe za
kilele cha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama
kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nane
Nzuguni Mkoani Dodoma
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akimkabidhi zawadi Bi. Lilian
Simon mmoja ya wakina mama walionyonyesha watoto wao kwa kufuata
maelekezo ya wataalamu na kuwezesha watoto wao kuwa na afya bora na
kukua vizuri.
Kikundi
cha ngoma za asili ya kigogo cha zepisa Hombolo kikitumbuiza wakati wa
sherehe za kilele cha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa
ya mama kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane
Nanne Nzuguni Mkoani Dodoma.
Vijana
wa bendi ya muziki ya Winners ya Mjini Dodoma wakionesha ufundi wa
kusakata muziki wakati wa sherehe za kilele cha Maadhimisho ya 23 ya
wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa
wiki kwenye viwanja vya Nane Nanne Nzuguni Mkoani Dodoma.
Bi. Lilian Simon akiwa amembeba Mwanae Dorcas David (3) akipongezwa
na Vijana wa bendi ya muziki ya Winners alipotoa ushuhuda wa faida ya
kumnyonyesha mtoto wake maziwa ya mama pekee hadi alipofikisha umri wa
miezi sita na baadae kuendelea hadi miaka miwili wakati wa sherehe za
kilele cha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama
kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nanne
Nzuguni Mkoani Dodoma
Bi.
Judina Deus Malya akiwa na watoto wake mapacha Noel na Nance Malya (4)
mara baada ya kutoa ushuhuda wa faida ya kuwanyonyesha watoto wake
maziwa ya mama pekee hadi walipofikisha umri wa miezi sita na baadae
kuendelea hadi miaka miwili wakati wa sherehe za kilele cha Maadhimisho
ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika
mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nanne Nzuguni Mkoani Dodoma
Baadhi ya Wananchi wa Dodoma waliofika kwenye viwanja
vya Nane Nane Nzuguni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo Chiku Gallawa
(hayupo pichani) wakati akitoa hotuba ya kuhitimisha Maadhimisho ya 23
ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa mwishoni mwa wiki.
Picha
ya pamoja baina ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa (katikati),
viongozi wa Mkoa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na wamama
walionyonyesha watoto wao kwa kufuata masharti ya wataalamu na watoto
wao wenye afya bora baada ya kumalizika kwa Maadhimisho ya 23 ya wiki ya
unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa mwishoni mwa wiki kwennye viwanja
vya Nane Nane Nzuguni Mkoani humo.
Picha
ya pamoja baina ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma, viongozi wa Mkoa na Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii ambao kwa pamoja wameshirikiana katika
maandalizi na kufanikisha Maadhimisho
ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa yaliyohitimishwa
mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nane Nzuguni Mkoani humo.
0 comments:
Post a Comment