Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mgombea
unaibu spika kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Tulia Ackson
Mwansasu, amekanusha madai kwamba amepewa nafasi hiyo kama pandikizi ili
aibebe Serikali.
Amesema
madai kuwa ataibeba Serikali kwa kuwa ni mbunge wa kuteuliwa hayana
msingi kwa kuwa haendi bungeni kumtumikia rais bali kuwatumikia
Watanzania.
Rais
John Magufuli Jumatatu wiki hii alimteua Dk. Ackson kuwa mbunge wa
kuteuliwa na kutengua nafasi yake ya naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali
aliyoteuliwa hivi karibuni na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.
“Ni
kweli nimeteuliwa na rais, lakini nakwenda kufanya kazi za Watanzania,
nikipata nafasi ya kuwa naibu Spika madai kuwa nitaibeba serikali hayapo
kwa kuwa nitafanya kazi za Bunge ambazo ni kuisimamia, kuishauri na
kuiwajibisha serikali,” alisema Dk. Ackson ambaye juzi usiku alipitishwa
kwa kauli moja na wabunge wa CCM kuwa mgombea wake wa unaibu spika.
Alisema ni vyema wabunge wakawa na imani naye na kumpa ushirikiano wa dhati ili atekeleze majukumu yake ipasavyo.
Katika
hatua nyingine, vita ya unaibu Spika wa Bunge la 11, imemalizika, baada
ya, Dk. Ackson, kupitishwa kwa kauli moja na wabunge wa CCM kugombea
nafasi hiyo.
Awali
kulikuwa na mvutano wa ndani kwa ndani baina ya wabunge wa chama hicho,
ambao waligawanyika kwa baadhi kumtaka Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan
Zungu.
CHANZO: MATUKIO DAIMA
CHANZO: MATUKIO DAIMA
0 comments:
Post a Comment