Mwenyekiti wa kikao cha
Bunge ambaye pia Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge amewataka
wabunge kujifunza kwa umakini namna bora ya kutumia kanini za Bunge.
Mwenyekiti Chengeamefanya
hivyo mara kadhaa alipokuwa akijibu miongozo ya wabunge kutoka vyama vya
upinzani wakiwamo Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea (CHADEMA), Mbunge wa
Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT) pamoja na Mbunge wa Singida Magharibi
Tundu Lissu (CHADEMA).
Kwa upande wa Kubenea
ameomba muongozo kuhusu mbwa walioingizwa Bungeni na askari polisi
wanaume kuwapekua wanawake jambo ambalo ahaliruhusiwi kwa kanuni ambapo
Mwenyekiti wa Bunge amemtaka mbunge huyo kutafuta kanuni nyingine ya
kupeleka ombi lake kama anadhani hoja yake ni ya msingi.
Kwa upande wa Lissu pamoja
na Zitto wenyewe wameomba miongozo kuhusu mpango wa serikali wa miaka
mitano uliowasilishwa na serikali kupitia wizara ya fedha,kwamba
umekiuka kanuni za bunge,ambapo mwenyekiti akawajibu kwamba mpango
haujakiuka na sii mara ya kwanza kufanya hivyo.
Aidha Mwenyekiti wa Bunge
ametoa rai kwa wabunge wote kuzisoma kanuni za bunge na kuzielewa na
mipaka yake katika namna bora ya kuendesha vikao hivyo vya Bunge.
Hata hivyo Kikao cha bunge
kimeendelea na shughuli zake huku wabunge wa kambi rasmi ya upinzani
wakirejea baada ya kugomea kushiriki katika mjadala wa kuijadili hotuba
ya Rais kwa kigezo cha shirika la utangazaji la Taifa kutorusha
matangazo ya moja kwa moja kuhusiana na mijadala hiyo.
0 comments:
Post a Comment