____________________
Kamati ya Kanuni ya Bunge iliyoundwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai hivi karibuni, leo imekutana Jijini Dar es
Salaam na Kuridhia mapendekezo ya mabadiliko katika muundo wa kamati za Bunge yaliyowasilishwa
na Mhe. Spika
ili kuendana na mabadiliko ya Muundo wa Wizara katika Serikali ya awamu ya
Tano.
Mabadiliko hayo ambayo
yamefanywa chini ya kanuni ya 155 (3) ya kanuni za Kudumu za Bunge yamezingatia
madaraka aliyonayo Spika kufanya marekebisho kwenye nyongeza za kanuni kwa
kushauriana na kamati hiyo.
Akizungumza na
wajumbe wa kamati hiyo Mh. Ndugai ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati hiyo amesema
amelazimika kufanya mabadiliko katika muundo wa kamati ili kuendana na
mabadiliko ya Wizara na kwa kuzingatia kuwa muundo wa kamati umetajwa kwenye
nyongeza ya nane.
Katika muundo huo
Kamati mbili mpya zimeundwa ambazo ni kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo na kamati
ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma.
Akifafanua kuhusu
maamuzi ya Kikao hicho, katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah amesema kikao
hicho kimekuwa na mafanikio makubwa na kuridhia mapendekezo ya Mhe. Spika kama
yalivyowasilishwa.
Aidha Dkt.
Kashililah aliongeza na kusema kuwa Kamati nyingine zimefanyiwa mabadiliko
kwenye majina na nyingine mbili kuunganishwa na kufanya kamati mpya za Bunge
kuwa kama ifuatavyo:
Kamati
zilizounganishwa ni:
·
Kamati
ya Huduma na maendeleo ya Jamii - imeunganishwa
kutoka iliyokuwa Kamati ya Maendeleo
ya Jamii na kamati ya Huduma za Jamii
·
Kamati
ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama – imeunganishwa
kutoka iliyokuwa Kamati ya Ulinzi na
Usalama na kamati ya mambo ya Nje.
Kamati
zilizofanyiwa Marekebisho madogo kwenye majina ni:
·
Kamati
ya Viwanda, Biashara na Mazingira (awali ilikuwa
Kamati ya Viwanda na Biashara)
·
Kamati
ya Ardhi, Maliasili na Utalii (awali ilikuwa Kamati
ya Ardhi, Maliasili na Mazingira)
·
Kamati
ya Utawala na Serikali za Mitaa (awali ilikuwa Kamati
ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa)
Kamati zilizobakia
kama ilivyokuwa awali ni pamoja na:
·
Kamati ya Uongozi,
·
Kamati ya Kanuni za Bunge,
·
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka
ya Bunge,
·
Kamati ya Katiba na Sheria
·
Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji,
·
Kamati ya Miundombinu
·
Kamati ya Nishati na Madini.
·
Kamati ya bajeti
·
Kamati ya Masuala ya Ukimwi
·
Kamati ya Hesabu za Serikali za
Mitaa (LAAC) na
·
Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC)
Wabunge wote
wanatakiwa kuwasili Dodoma tarehe 20 Januari, 2016 tayari kwa kuanza Vikao vya
Kamati kabla ya Mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 26 Januari, 2016.
Imetolewa
na,
Kitengo
cha Habari, Elimu na Mawasiliano.
Ofisi
ya Bunge,
S.L.P 9133,
DAR ES SALAAM
15 Januari, 2016.
0 comments:
Post a Comment