Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Mh. George Simbachawene amemvua madaraka Mkurugenzi Mtendaji wa
Manispaa ya Dodoma, Bw. Augustino Kalinga kufuatia kuruhusu ofisi yake
kuwachangisha wazazi michango ambayo serikali imezuia katika kutoa elimu
ya msingi bila malipo.
Mh.
Simbachawene alifikia uamuzi huo jana mjini Dodoma wakati akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na serikali baada ya
kugundua kuwa manispaa ya Dodoma imesambaza barua kwa walimu wakuu wa
shule za msingi ambazo zimeagiza kuwatoza wazazi michango ya maji, umeme
na mlinzi ambayo imekatazwa na serikali.
Amesema
kuwa Bw. Kalinga amevuliwa madaraka yake baada ya kubainika kuwa
ameshindwa kuwasimamia watumishi walio chini yake hadi kusababisha
kuandika barua na kusambaza kwa walimu wakuu wa shule za msingi katika
manispaa ya Dodoma ambayo inatofautiana na maelezo ya serikali yaliyopo
kwenye mwongozo.
Aidha,
amebainisha kuwa katika mwongozo wa elimu ya msingi uliotolewa na
serikali unafafanua majukumu ya wazazi na walezi ambayo wanatakiwa
kuyafanya kuwa ni pamoja na sare za shule, vifaa vya michezo na vya
kujifunzia pamoja na matibabu na chakula.
Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment