Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Akson akitoa maelekezo wakati wa mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.
Mbunge
wa Viti Maalum Tabora mjini Mhe. Mwanne Nchemba (CCM) akichangia hoja
wakati kujadili hoja ya Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi,
Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene
na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge
wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema (CHADEMA) akichangia hoja wakati
kujadili hoja ya Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na
Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene na Angella
Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma
Wabunge
wakifuatilia mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais,Tamisemi,
Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George Simbachakene
na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo Bungeni mjini Dodoma
Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiongea na Mbunge wa Iringa Mjini
Mchungaji Peter Msigwa (katikati) mara baada ya kumalizika mkutano wa
Bunge leo mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Utumishi Seleman Jafo akiwa katika
picha ya pamoja na wageni wake waliomtembelea leo Bungeni, mjini Dodoma.
WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwa katika picha
ya pamoja na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo Bungeni,
mjini Dodoma.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma)
………………………………………………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amewapongeza wabunge kwa kushiriki
vizuri mashindano ya Muungano yaliyofanyika Zanzibar na kurudi salama
mjini Dodoma kuendelea na majukumu yao.
Pongezi hizo za Spika zimetolewa
leo Bungeni Dodoma na Naibu Spika Dkt. Tulia Akson kwa niaba ya Spika
alipokuwa akitoa matangazo kabla ha kuahirisha shughuli za Bunge hadi
jioni ambapo Bunge linaendelea kujadili hoja ya Hotuba za Ofisi ya
Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora inayoongozwa na Mawaziri George
Simbachakene na Angella Kairuki iliyowasilishwa mapema leo.
Timu za Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania zilizoshiriki mashindano hayo ni timu za mpira wa
miguu na pete ambapo timu ya mpira wa pete imefanya vizuri kwa kuishinda
timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa magoli 18 kwa magoli 15
wakati timu ya mpira wa miguu zilitoka sare ya kufungana goli 1:1
Kushiriki kwa Wabunge katika
mashindano hayo yamelenga kuimarisha udugu uliopo kati ya pande mbili za
Muungano na kuwapa fursa Wabunge kufanya mazoezi kwa ajili ya kujenga
na kuimarisha afya zao.
Aidha, michezo kwa Wabunge inatoa
nafasi kubwa ya ushirikiano ambayo ni kielelezo cha msingi kinachozaa
Viongozi bora wanaotokana na sekta ya michezo.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wanafursa kubwa ya kufanya mazoezi mbalimbali katika kujenga na
kuimarisha timu za Bunge hilo ili kujenga pia ujirani mwema.
Ushiriki wa Wabunge kwenye
mashindano siyo mara ya kwanza, Wabunge hao hushiriki michezo
mbalimbali, wanashiriki mpira wa miguu wakiwa watani wa Jadi wa timu za
Simba na Yanga, Februari 4, 2012 walishiriki mazoezi ya viungo
yaliyoendeshwa na klabu inayojulikana kama “Kitambi noma” kutoka mjini
Unguja kwa kuzingatia Bunge lina eneo mahususi la kufanyia mazoezi
mazoezi ya viungo (Gym).
0 comments:
Post a Comment