Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama ameiagiza Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya
Waziri Mkuu kufanya tathimini ya hali halisi za athari zilizosababishwa
na ndege aina ya kwerea kwerea katika mashamba ya mtama na uwele
yaliyopo Mkoani Dodoma katika Wilaya Bahi.
Waziri
Mhagama aliyasema hayo wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Katiba na Sheria cha Kupitisha Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
kilichofanyika jana katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini
Dar es Salaam.
Kikao
hicho kiliibua hoja za wajumbe ikiwemo hoja iliyo bainisha athari za
maafa kwa wakazi wa Wilaya ya Bahi kuhusu ukosefu wa chakula baada ya
mashamba yao kuvamiwa na ndege waharibifu aina ya Kwerea kwerea.
Hoja
hiyo iliibuliwa na Mbunge wa Bahi Bw. Omar Badwel alisema wananchi wake
wapo katika wakati mgumu hivyo wanahitaji msaada kutoka serikalini kwa
kuwa mazao yao yamevamiwa na ndege hao.
“Kwerea
kwerea wamekuwa ni changamoto kwa wakazi wa wilaya yangu hususani
maeneo ya Manyoni ninaomba serikali kupitia Idara ya Maafa isaidie kwa
kuwapa chakula na mbegu Wananchi ili waweze kujikimu na kuitatua
changamoto hiyo”Alisema Badwel.
“Mazao yaliyoshambuliwa na kuharibiwa na ndege aina ya kwerea kwerea ni mazao ya mtama na uwele, Alisisitiza”.
Waziri
Mhagama alisema anatafuta uwezekano wa kuona umuhimu wa kushirikisha
Wizara ya kilimo na Mifugo kwa kuangalia namna zinavyoweza kushirikiana
kuondoa wadudu waharibifu wa mazao mkoani Dodoma.
“Serikali
itafanya tathmini kwa waathirika hao wa maafa Wilayani Bahi, ni vizuri
Idara ya Maafa ifanye hivyo haraka ili kusaidia kunusuru hali ya wakazi
wa Dodoma”Alisisitiza Mhagama.
Waziri Mhagama alimpongeza Mhe.Badwel kwa kuwajali wananchi wa Bahi kwa kuibua jambo muhimu hivyo aliahidi kulitafutia ufumbuzi wa haraka.
“Suala
hili ni muhimu kwa kuwa linagusa maisha ya Wananchi moja kwa moja sisi
kama serikali tumelichukua kwa uzito na tutahakikisha Idara ya maafa
inatembelea maeneo husika kwa ajili ya kufanya tathimini za haraka kwa
waathirika waliopoteza mazao yao ili kujua namna tunavyoweza kutoa
msaada wa haraka katika maeneo husika ” alisema Mhagama.
Awali;
kikao hicho kililenga kupitia na kujadili bajeti ya Ofisi ya Waziri
Mkuu yenye fungu namba 25 (Ofisi Binafsi ya Mhe.Waziri Mkuu), 37(Sera,
Uratibu a Bunge), 15 na 65 (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) na
fungu 27 na 61 (Tume ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume ya Uchaguzi.
0 comments:
Post a Comment