Naibu
Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Ashatu Kijaji akijibu maswali
mbalimbali kuhusu Benki ya TIB na TADB katika kupunguza umaskini, leo
Bungeni mjini Dodoma.
Na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dodoma.
Hadi
kufikia mwaka jana (2015) Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB)
imewawezesha Watanzania wengi kupambana na umaskini kwa kutoa mikopo ya
zaidi ya shilingi bilioni 550 katika sekta mbalimbali za kiuchumi.
Taarifa
hiyo imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Ashatu Kijaji wakati akijibu swali toka kwa Mbunge wa
Karagwe, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) lililotaka kujua Serikali ina
mpango gani wa kuhakikisha kuwa Benki za TIB na TADB zinajielekeza
kwenye utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Mhe.
Kijaji ameeleza kuwa, madhumuni ya kuanzishwa kwa benki ya TIB na TADB
kama benki za maendeleo ni kutoa mikopo ya muda wa kati na muda mrefu
kwa lengo la kufadhili miradi ya kimkakati, hivyo katika kutimiza azma
ya kufadhili miradi ya kimkakati ya kufungua fursa za kiuchumi na
kupunguza umaskini, TIB imetoa mikopo katika maeneo ya miji kupitia NHC,
Viwanda vya kubangua korosho, maghala, mabomba ya maji, sukari na
kilimo cha miwa, kukoboa na kusindika kahawa, kusindika matunda, mifuko
ya kuhifadhia mazao na nyaya za umeme; vinu vya pamba na uzalishaji wa
mafuta yatokanayo na mbegu za pamba na hoteli.
Aidha,
TIB imetoa mkopo wa shilingi bilioni 489.2 kwa ajili ya utekelezaji wa
miradi 181 ya kusambaza umeme vijijini kupitia REA na kaya 257,000
zimenufaika na mradi huo. Pia vikundi 17 vya wachimbaji wadogo wadogo
vimenufaika na mikopo jumla ya shilingi bilioni 8.
“Mikopo
ya TIB kwa sekta na taasisi mbalimbali imesaidia kwa kiasi kikubwa
kutoa ajira na kuendeleza zilizopo. Pia mikopo ya TIB imetumika kuongeza
uzalishaji wa bidhaa zinazouzwa nje kama vile maua, kahawa na dhahabu”,
alisema Kijaji.
Aliongeza
kuwa pamoja na benki ya Kilimo kuchelewa kuanza kutoa mikopo, ni wazi
kuwa benki ya TIB imejielekeza kwenye utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi
ya CCM pamoja na utekelezaji wa Mipango na mikakati mbalimbali ya
maendeleo ikiwemo Dira ya Taifa ya 2025, FYDB, SDGs 2030 pamoja na
Afrika 2063.
TIB
imewekeza katika mashirika ya umma kama vile Shirika la Reli (TRL), pia
imeiwezesha TPDC katika mradi wa gesi na kuipatia Shirika la Ugavi
Umeme Tanzania (TANESCO) mkopo kwa ajili ya fidia kwa wananchi ili
kuweka njia mpya ya kusafirisha umeme.
0 comments:
Post a Comment