Na. Immaculate Makilika- Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema katika kipindi cha uongozi wake atahakikisha Serikali inahamishia makazi yake mjini Dodoma.
Amesema hayo leo, wakati alipokuwa akihutibia wajumbe wa Chama cha Mapinduzi(CCM) katika Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama hicho uliofanyika mjini Dodoma mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti.
“Nitahakikisha
katika awamu ya uongozi wangu, Serikali inahamia Dodoma, najua viongozi
wengine wote nao watanifata, kwa kuwa sasa miundombinu ya Dodoma
inaweza kukidhi mahitaji yote” alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha miezi nane ya uongozi wake chini ya Serikali ya Awamu ya Tano ameweza kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuanza kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Akiongelea
maeneo ya utekelezaji katika kipindi chake Dkt. Magufuli alisema kuwa
mpaka sasa Serikali imefanikiwa kusimamia suala la utoaji wa elimu bure
kwa shule za Msingi na Sekondari nchini na kuwezesha udahili kuongezeka
zaidi tofauti na miaka iliyopita.
Aidha
Dkt. Magufuli alisema kuwa Serikali yake pia imefanikiwa kwa kiasi
kikubwa katika ukusanyaji wa mapato ya serikali hali itakayosaidia
kuimarisha utoaji wa huduma muhimu za jamii.
Aidha, Serikali ya Awamu ya Tano imeagiza ndege mbili mpya zinazotarajiwa kuwasili nchini Septemba mwaka huu,
Rais
Dkt. Magufuli aliongeza kuwa Serikali yake kwa kushirikiana na Serikali
ya Uganda wamefanikiwa kujenga bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima
katika ziwa Alberti nchini Uganda kwenda bandari ya Tanga ambapo mafuta
hayo yatasafirishwa sehemu mbalimbali duniani na bombahilo litazalisha zaidi ya ajira 20,000.
Vile vile, Rais Magufuli alisema kuwa Serikali yake imeweza kurudisha nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma na kuweza kuondoa watumishi hewa waliokuwa na waliokuwa wamefikia 12,500,na kuongeza
kuwa kwa mwaka huu Serikali imetenga fedha za matumizi jumla ya
shilingi trilioni 29.5, ambapo asilimia 40 ya fedha hizo zitapelekwa
katika kutekeleza shughuli za maendeleo.
Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ulihudhuriwa na wajumbe zaidi 2,000 ulimpitisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mshindi na Mwenyekiti wa Chama hicho kwa kura 2398 kati ya kura 2398 zilizopigwa ikiwa ni sawa na asilimia 100.
Rais Magufuli anakuwa Mwenyekiti wa awamu ya Tano baada ya kupokea
uongozi huo kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho anayemaliza muda wake
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka
10.
0 comments:
Post a Comment