Na.
Nasra Mwangamilo, Silvia Hyela
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Tawala za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameuagiza Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuhakikisha inakamilisha
ujenzi na ukarabati wa vyumba vya
madarasa ya shule ya msingi Chang’ombe, ifikapo tarehe 10 Januari, 2017 kabla
ya msimu wa masomo kuanza.
Mhe. Jafo alisema serikali
kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) imetoa
jumla ya shilingi Milioni 192 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 8 vya madarasa na ukarabati
wa majengo machakavu katika shule ya msingi Chang’ombe na kuwataka watendaji
hao kutumia vizuri fedha hizo zilizotolewa na serikali.
Mhe. Jafo alitoa agizo hilo leo tarehe 03 Novemba, 2016
wakati alipofanya ziara ndogo ya kutembelea Kata ya Chang’ombe ambapo katika
ziara hiyo alibaini changamoto
mbalimbali zinazoikabili shule hiyo zikiwemo upungufu wa madarasa na matundu ya
vyoo.
“Natoa agizo kwa Afisa Mipango na Kaimu Mkurugenzi wa
Manispaa, ifikapo tarehe 10 Januari, 2017, ujenzi wa majengo haya uwe
umeshakamilika na muhakikishe shule yote inakuwa mpya. ” Alisisitiza Mhe. Jafo.na kuongeza kuwa
angependa kazi hiyo ifanyike ndani ya muda na kutojengwa chini ya kiwango cha
ubora.
Aidha, Naibu Waziri
Jafo alionyesha kutoridhishwa na taarifa
za ujenzi wa zahanati ya kata ya Chang’ombe ambayo taarifa zilizotolewa
zilionyesha kuwa hazikuwa sahihi ukilinganisha na idadi ya fedha zilizotolewa
kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo.
“Sijaridhishwa kabisa na
ujenzi unaoendelea katika zahanati hii na siamini kama kulikua na usimamizi
mzuri, nataka niletewe taarifa inayoambatana na taarifa ya mkandarasi
aliyehusika na ujenzi pamoja na mchakato wa manunuzi ya vifaa na maendeleo ya ujenzi
ili nijiridhishe na suala hili ”aliagiza Naibu Waziri Jafo.
Katika ziara hiyo, Mhe. Jafo alipata nafasi ya
kuzungumza na watumishi wa Manispaa ya Dodoma na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia umuhimu wa
mahitaji ya wananchi na kuyawekea kipaumbele mambo ya msingi ikiwamo huduma za
afya na elimu lengo likiwa ni kuhakikisha watumishi wa Serikali za Mitaa
wanakua watumishi wa mfano kwa utendaji mzuri.
0 comments:
Post a Comment