Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda
akizungumza na waandishi wa habari kuelezea dhamira ya ujio wa Waziri
Mkuu wa Ethiopia nchini Tanzania mapema leo katika Ukumbi wa Benjamin
Mkapa Mjini Dodoma.(Picha Zote Na Mathias Canal)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akisikiliza na kujibu maswali ya waandishi wa habari mapema leo katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa Mjini Dodoma
Baadhi ya Wakurugenzi wa Manispaa za Jiji La Dar es salaam wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda wakati akizungumza na Waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda wakati akielezea ujio wa Waziri Mkuu wa Ethiopia
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea ujio wa Waziri Mkuu wa Ethiopia katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa Mjini Dodoma

Mkapa Mjini Dodoma.
Na Mathias Canal, Dodoma
Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe Hailemariam Desalegn anataraji kuwasili
nchini kesho Machi 31, 2017 katika uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere kwa ziara ya Siku tatu kwa kuitikia Mwaliko wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ambaye ndiye atakuwa
mwenyeji wake.
Taarifa ya ujio wa waziri Huyo Mkuu wa Ethiopia imetolewa hii Leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea dhamira ya ujio huo katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa Mjini Dodoma.
Rc Makonda ameeleza
kuwa Mhe Desalegn anataraji kuwasili nchini saa tatu kamili asubuhi
Machi 31, 2017 hadi April 1, 2017 ambapo atakuwa nchini kwa shughuli
mbalimbali za kidiplomasia zinazogusa nyanja muhimu za kiuchumi,
Biashara, na Ushirikiano baina ya Nchi ya Ethiopia na Tanzania.
Mhe
Makonda alisema kuwa Waziri huyo Mkuu wa Ethiopia pamoja na shughuli
hizo za kidiplomasia pia atasaini mikataba mitatu, Kutembelea bandari na
kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli.
Makonda
alisema kuwa Tanzania itapata fursa ya kujifunza mambo mengi kupitia
kwa ugeni huo juu ya kukabili changamoto mbalimbali zinazolikabili bara
la Afrika katika masuala ya kilimo cha kisasa katika maeneo yenye uoto
wa asili wenye changamoto kama milima hapa nchini Tanzania.
"Tutajifunza
mengi sana kama ilivyo kwa Ethiopia ambao mbali ya kukabiliwa na uoto
usio rafiki wa milima na miinuko mikali kwa asilimia kubwa bado wameweza
kutumia vyema maeneo machache ya tambarare na Kuwekeza kufanya kilimo
cha kisasa na kuzalisha chakula kwa wingi, hivyo tutapata ufahamu pia
katika mambo haya muhimu" Alisema Mhe Makonda
Kwa
niaba ya wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda amesema
kuwa uongozi wa Mkoa wake unamkaribisha nchini Tanzania kwani ujio wake
utaibua zaidi fursa za kukuza uchumi na Maendeleo.
Hata
hivyo amesema kuwa Ethiopia imepiga hatua kubwa kwenye usafiri wa Anga
Duniani hivyo kupitia rekodi hiyo nzuri Tanzania pia itapata wasaa
wakujifunza mambo mengi katika sekta hiyo.
0 comments:
Post a Comment