Na. Mwandishi Wetu
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama amezindua mfumo mpya wa Kielektroniki wa
Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya
Viongozi Wakuu ulianzishwa kwa lengo la kusaidia upatikanaji na utoaji
wa taarifa za utekelezaji kupitia mfumo wa kisasa (kidigitali).
Akizindua
mfumo huo wakati wa mkutano na waandishi wa habari Machi 28, 2017
Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni, Waziri alieleza umuhimu wa mfumo
huo kuwa umejikita katika kusaidia Viongozi Wakuu kupata Taarifa za
utekelezaji wa Maagizo yao na yale yaliyoelekezwa katika Ilani ya
Uchaguzi ya Chama Tawala.
“Mfumo
huu utasaidia sana katika kufuatilia shughuli za Serikali ikiwa ni
pamoja na ufuatiliaji wa maazigo yote na ahadi zilizotolewa ili kuona
utekelezaji wake kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa awali” Alisema
Mhe.Waziri.
Aidha
mfumo utasaidia pia Ofisi ya Waziri Mkuu kuongeza ufanisi wa uratibu na
ufuatiliaji wa shughuli za kila siku za Serikali kwakuwa taarifa zote
zitapatikana kwa wakati na takwimu za uhakika.
Alibainisha
kuwa, kuanzishwa kwa mfumo ni moja ya sehemu ya kuondoa changamoto
kadhaa ikiwa ni kuongeza ufanisi maeneo yetu ya kazi “kuanzishwa kwa
mfumo huo kutatua changamoto za uchelewashwaji wa taarifa, na
kutowajibika kwa ujumla na kuleta ufanisi kazini”.Alisisitiza waziri.
Aidha
kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Hamisi Mwinyimvua
alibainisha kuwa mfumo umepitia hatua zote muhimu ikiwa ni pamoja na
kuwashirikisha Mawaziri wote, Makatibu Wakuu wote, Wasaidizi wa Mhe.Rais Jonh Magufuli na Watendaji wa Serikali.
Kwa
kumalizia Waziri alipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na
Wakala wa Serikali Mtandao kwa kuona umuhimu wa kuwepo kwa mfumo huu na
kutoa rai kwa Watendaji wote wa Serikali kuutendea haki kwa kufanya kazi
bila uzembe wowote. “rai
yangu kwa Watumishi wa Umma wote Nchini kuwajibika kwa kufanya kazi
kwani kupitia Mfumo huu, mzembe atajulikana na mchapa kazi atajulikana.
Na ikumbukwe tu, wazembe na wavivu hawana nafasi katika Serikali ya
Awamu ya Tano”.
0 comments:
Post a Comment