Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akipokea shada la maua
kutoka kwa mtumishi Joyce Mtuma mara baada ya kuwasili Wizarani mjini
Dodoma.
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akiangaalia kadi ya
Pongezi iliyoasiniwa na watumishi wa wizara mara baada ya kuwasili
Wizarani mjini Dodoma
WaziriwaKatibanaSheriaMhe.
Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana naNaibu Katibu Mkuu Bw. Amon
Mpanju mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma
Waziri
wa Katiba na SheriaMhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana na Jaji
mfawidhi Kanda ya Dodoma Mhe. Mwanaisha Kwariko alipowasili Wizarani
mjini Dodoma
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisikiliza maelezo
mbalimbali alipokutana na watendaji wa Wizara na Mahakama katika ukumbi
wa mikutano Wizarani mjini Dodoma
Waziri
wa Katiba na Sheria Prof.Palamagamba Kabudi amewasili katika Ofisi za
Makao makuu ya Wizara zilizoko ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma na
kulakiwa na watumishi wa Wizara walioko makao makuu ya Serikali mjini
Dodoma.
Prof
Kabudi aliapishwa tarehe 24/03/2017 Ikulu jijini Dar Es Salaam kuchukua
nafasi hiyo baada ya Mhe.Rais kufanya mabadiliko madogo kwenye Baraza
la Mawaaziri ambapo Dkt. Harrison Mwakyembe alihamishiwa Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Nje ya
Ofisi za Wizara Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi alilakiwa na Naibu Katibu
Mkuu, Bw. Amon Mpanju, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw.
Aloyce Mwogofi, Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma na wafanyakazi wengine wa
Wizara waliopo Makao Makuu ya Serikali mjini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment