Waziri
wa Afya, maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa
kwanza kulia akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa kampeni ya yautunzaji
wa mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI”uliofanyika mjini leo mjini
Dodoma.
Waziri wa Afya, maendeleo yaJamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akiwa amebeba nembo inayoashiria uzinduzi wa kampeni ya kutunza mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI” uliofanyika mjini Dodoma , wengine ni wadau mbalimbali wa mazingira pamoja na baadhi ya wabunge.
Waziri wa Afya, maendeleo yaJamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akiwa amebeba nembo inayoashiria uzinduzi wa kampeni ya kutunza mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI” uliofanyika mjini Dodoma , wengine ni wadau mbalimbali wa mazingira pamoja na baadhi ya wabunge.
Waziri
wa Afya, maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akizungumza mbele ya wabunge na wadau mbalimbali wa afya na mazingira
hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa kampeni ya yautunzaji wa mazingira
ijulikanayo kama “NIPO TAYARI”iliyofanyika leo mjini Dodoma.
Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akiteta jambo na Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Suleiman Jaffo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya yautunzajiwa mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI” uliofanyika mjini leo mjini Dodoma. Pichana Ally Daud-WAMJW DODOMA.
Na Ally Daud-WAMJW DODOMA
SERIKALIi
imedhamiria kuboresha kiwango cha vyoo bora mjini na vijijini kutoka
asilimia 35 hadi asilimia 55 kufikia mwaka 2025 ili kujenga taifa lenye
afya bora na lisilo na maambukizi ya magonjwa yatokanayo na uchafu wa
vyoo.
Akizungumza
hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya utunzaji wa mazingira ijulikanayo
kama “NIPO TAYARI” Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imepania kufikisha asilimia ya
ubora wa vyoo mpaka kufikia 2030.
“Hatua
hii itafikiwa endapo kwa pamoja tutasukuma mbele ajenda ya usafi wa
mazingira kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hasa katika ujenzi wa
vyoo bora,utupaji salama wa taka ngumu,upatikanaji wa maji salama kwa
mikono miwili” alisema Waziri Ummy.
Aidha
Waziri Ummy amesema kuwa yapo mafanikio yaliyofikiwa katika kupunguza
kasi ya watu kujisaidia ovyo tabia ambayo ni kisababishi cha maambukizi
ya magonjwa mengi katika jamii.
Mbali
na hayo Waziri Ummy alitoa rai kwa wanasiasa wenginekushirikiana na
wananchi katika majimbo yao ilikusukuma kwa vitendo ajenda ya Usafi wa
Mazingira nchini .
Kwa
upande wake Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Bw. Suleiman Jaffo amesema kuwa watanzania wa wa mijini na
vijijini wawe mstari wa mbele katika kuhakikisha wanatumia vyoo bora
kila kaya ili kuepuka magonjwa ya kuambukiza.
Naye
Naibu Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kuwa
ili kuendana na kasi hiyo wamejipanga kuhakikisha shule zote za msingi
na sekondari nchini zinapata maji safi na salama kwa wakati sahihi.
0 comments:
Post a Comment