Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano imesema
itajenga daraja la juu kwa ajili ya kivuko cha waenda kwa miguu(Over
head Pedestrian Bridge) eneo la Kawe Bondeni.
Hayo yamesemwa Bungeni leo na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Mhe.Isack Kamwelwe aliyekuwa akijibu swali la Mbunge wa Kawe Mhe.Halima
Mdee kwa Niaba ya Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.
“Tatizo la kivuko cha waenda kwa miguu eneo la Kawe Bondeni hadi
Jeshini Kata ya Mbezi Juu na Kawe Tayari limeshapatiwa
ufumbuzi”,Aliongeza Mhe.Kamwelwe.
Amesema kwa sasa Mkandarasi wa kujenga daraja hilo yupo kwenye hatua za maandalizi ya kuanza ujenzi katika eneo hilo muhimu.
Aidha Serikali ina mpango wa kuweka taa za kuongozea magari katika
Barabara ya Mwenge-Tegeta ambapo Mkandarasi ameshapatikana wa kuweka
taa hizo katika makutano ya Afrikana na anatarajia kuanza kazi wakati
wowote.
Mbali na Hayo tatizo la Udogo wa mapokeo na matoleo ya maji ya mvua
yanayosababisha kero katika eneo la Makonde hadi Mbuyuni,Serikali
inakamilisha taratibu za kusaini mkataba wa ujenzi wa mtaro mkubwa eneo
la Mbezi Samaki ambao utatatua kero ya barabara kujaa maji nyakati za
mvua.
“Serikali ya Awamu ya Tano ni makini sana na itahakikisha
changamoto hizi inazifanyia kazi ili wananchi waweze kutumia barabara
zetu vyema”Aliongeza Mhe.Kamwelwe.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment