Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mgombea aliyeshinda nafasi ya Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Jumannne Ngede (CCM) akitoa neno kwa wajumbe mara baada ya kushinda nafasi hiyo kufuatia uchaguzi uliofanyika jana katika ukumbi wa Manispaa hiyo.
Mgombea aliyeshindwa nafasi ya Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Samwel Mziba (CHADEMA) akitoa neno kwa wajumbe mara baada ya matokeo kutangazwa kufuatia uchaguzi uliofanyika jana katika ukumbi wa Manispaa hiyo.
Na Ramadhani Juma-Ofisi ya Mkurugenzi
NAIBU
Meya wa Manispaa ya Dodoma aliyemaliza muda wake Jumanne Ngede
amefanikiwa kutetea nafasi yake katika uchaguzi uliofanyika jana katika
ukumbi wa Manispaa ya Dodoma ambapo wajumbe 56 walishiriki uchaguzi huo.
Katika
uchaguzi huo Ngede ambaye ni Diwani wa Kata ya Chamwino kupitia Chama
Cha Mapinduzi (CCM) alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 47 dhidi ya
mpinzani wake kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Samwel
Mziba ambaye ni Diwani wa Kata ya Hazina aliyepata kura 9.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Dodoma ambaye ni Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la
Dodoma Mjini Godwin Kunambi alimtangaza rasmi Ngede kuwa Naibu Meya wa
Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.
Baada
ya kufanikiwa kutetea nafasi yake, Ngede aliwashukuru wajumbe kwa
kumchagua kwa kura nyingi jambo linaonesha kuwa wana imani kubwa na
utendaji wake na kwamba ataendelea kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa na
kwa kushirikiana na Madiwani wote.
Kwa
upande wake, mgombea aliyeshindwa Samweli Mziba aliwashukuru wajumbe na
kumpongeza mshindi huku akidai uchaguzi umepita na sasa ni kuchapa kazi
tu.
0 comments:
Post a Comment