Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akionja asali katika moja ya mabanda ya maonyesho ya nanenane
kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akitazama bidhaa za mbogamboga katika banda la Wilaya ya
Kondoa katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mkoa wa Singida
katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akionyeshwa shamba la mahindi lilostawi vizuri katika maonyesho
ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akipokea zawadi ya kikapu
kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza
Mkoa wa Dodoma SACP Julius Sang’udi alipotembea banda la jeshi la
magereza kujionea bidhaa wanazotengeza katika maonyesho ya nanenane
kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya
Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akitoka katika banda la Tume
ya taifa ya Umwagiliaji, kushoto
kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu katika maonyesho ya
nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni,
Manispaa ya Dodoma.
Maonyesho ya nane nane yanatakiwa kuweka alama chanya na kuwa na sura ya mabadiliko yanayoonekana kwa macho
kwa wakulima na wafugaji wanaoshiriki pamoja na wananchi wanaopata huduma na bidhaa katika maonyesho hayo.
Mgeni
rasmi katika Ufunguzi wa maadhimisho ya nanenane kanda ya kati ambaye
ni Mkuu wa Mkoa wa Singida
Dkt. Rehema Chimbi ametoa rai hiyo mapema jana kwa wakulima, wafugaji na
washiriki wakati akifungua rasmi maonyesho hayo huku akiwataka
washiriki hao kuitumia fursa hiyo kwa manufaa zaidi.
“Ni
vizuri maadhimisho ya Mwaka huu yakaonesha mabadiliko chanya kwa
washiriki mliojitokeza katika kuonesha
bidhaa zenu mbalimbali na pia kwa wale wote waliofika kwaajili ya
kununua au kupata maelezo ya matumizi ya bidhaa hizo, wapate kitu
tofauti kitakachooneka katika maisha yao”, amesema.
Dkt Rehema Nchimbi ambaye ametumia muda usipungua dakika 45 kusisitiza umuhimu wa kuwekeza katika kilimo
na ufugaji wenye tija ili kuendana na falsafa ya serikali ya awamu ya Tano inayo himiza zaidi Uchumi wa Viwanda.
Aidha
ameliomba Jeshi la Magereza na wawekezaji wote wa ndani na nje ya Nchi
wafike kuwekeza katika mikoa
ya Singida na Dodoma na kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
watahakikisha wanatengeneza mazingira rafiki kwa kila atakayekuwa tayari
kuwekeza katika Mikoa hiyo.
“Nimepita
kwenye banda la Jeshi la Magereza na kuona bidhaa nyingi sana
zilizotengenezwa na Ngozi na wamenihakikishia kuwa kiwanda chao kina
uwezo wa kununua ngozi yote inayopatikana katika Mikoa ya Singida na
Dodoma hivyo ni vizuri tutumie hiyo kama fursa” ameongeza
Dkt Nchimbi.
Dkt
Nchimbi amesisitiza kuwa Mikoa ya Singida na Dodoma haina ukame na ndio
maana hivi sasa ameanzisha
mpango maalum wa kilimo cha umwagiliaji kwakuwa watafiti
wamewahakikishia kuwa mikoa hiyo ina kiwango kikubwa cha maji ardhini
huku yakiwa karibu na uso wa ardhi.
Pia amewataka wananchi wa Mikoa ya Singida na Dodoma kuacha kabisa kukata miti kwa kisingizio cha kujikwamua
kiuchumi kwasababu kuna njia nyingi sana za kuondokana na hilo badala ya kuharibu misitu.
“Kule Singida nimeanzisha kampeni inayojulikana kama ‘ACHIA SHOKA, KAMATA MZINGA’ ambayo inampa
mwananchi nafasi ya kuamua kuacha kukata mti na badala yake anafuga
nyuki jambo linalomsaidia kujikwamua kiuchumi kwa muda mrefu zaidi
kwasababu unaweza kuukata mara moja tu lakini mzinga unaweza kuutundika
mara nyingi kadri uwezavyo”.
Dkt.
Nchimbi alimalizia hotuba yake kwa kuwasisitiza maafisa kilimo kupeleka
kalenda za kilimo katika ngazi
zote kuanzia ngazi ya kijiji ili iwe rahisi kwa Mkulima kujua aina ya
mazao anayoweza kulima kwa Mwaka husika badala ya kumsubiri Mkulima
apate madhara kwanza ndipo aje apewe elimu ya mazao aliyotakiwa kulima
kwa mwaka husika.
Maadhimisho ya 21 ya Sikukuu ya Wakulima na Wafugaji maarufu kama NANENANE yamefunguliwa rasmi tarehe 3
Agost 2017 kwa kanda ya kati inayojumuisha mikoa ya Singida na Dodoma.
0 comments:
Post a Comment