Imeandikwa na Sifa Lubasi, Dodoma
MAONESHO ya saba ya kitaifa ya mifugo juzi yalitia fora katika uwanja
wa maonesho ya kilimo Nzuguni Dodoma kutokana na mifugo iliyoletwa
kwenye maonesho hayo kuwa na afya nzuri na wenye kutoa maziwa mengi.
Miongoni wa vivutio hivyo ni ng’ombe dume aliyepewa jina la
Mang’wengw’e ikiwa na maana ya mtemi. Ng’ombe huyo ni mchanganyiko wa
golani na ng’ombe wa asili, ambapo ng’ombe huyo ni chifu katika kijiji
cha Kapiti Kata ya Mhalala Wilaya ya Manyoni mkoani Singida Katika
maonesho hayo yaliyozinduliwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk
Charles Tizeba (pichani), wafugaji wa mikoa ya Dodoma, Morogoro, Singida
na Pwani walipeleka mifugo yao katika maonesho hayo.
Miongoni mwa wafugaji walioleta mifugo yao Kedmond Makwayu kutoka
Gulwe wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, alionesha ng’ombe wake mwenye
mchanganyiko wa Mpwapwa na Golan mwenye uzito wa kilo 880 huku akitaja
gharama ya kumpandisha ng’ombe jike ni Sh. 30,000 Pia mfugaji kutoka
katika wilaya ya Chemba, Idris Noti alionesha ng’ombe dume aina ya
Tengeru mwenye uzito wa kilo 450 mwenye miaka mitano ambaye mpaka sasa
amezalisha ndama 20 na gharama za kupandisha jike ni Sh 10,000.
Mfugaji kutoka Itigi, Jihumbi Madeni alikuwa na ng’ombe wa asili
mwenye kilo 550. Aidha ng’ombe kutoka Ranchi ya Kongwa ambaye ni dume
mwenye jina la Mahinyika mwenye kilo 790 ambaye mpaka sasa amezalisha
zaidi ya ndama 200. Mfugaji Valentino Kombo kutoka Kongwa alikuja na
ng’ombe dume mwenye uzito wa kilo 970.
Mfugaji kutoka ranchi ya Rushu iliyopo Kisarawe Pwani alikuja na
ng’ombe mwenye kilo 831 huku Taasisi ya Utafiti ya Tarili Mpwapwa ikija
na ng’ombe aina ya Singida white mwenye kilo 450 na Iringa Red mwenye
kilo 360.
Pia ng’ombe kutoka kampasi ya Mpwapwa aliyepewa jina la mkufunzi wa
Chuo hicho, Kitinga mwenye kilo 430 na ana uwezo wa kutoa lita 21 za
maziwa kwa siku. Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya KIlimo, Mifugo na
Uvuvi, Dk Mary Mashingo alisema Tanzania ina rasilimali kubwa ya mifugo
na kutaka wafugaji kubadilika na kufuga kisasa.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment