Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Erasto Ching’oro WAMJW
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekutana na
wadau wa masula
ya jinsia mkoani Dodoma wanaokutana kudurusu Sera ya Mendeleo ya
Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 ili kuiboresha kwa kuzingatia mazingira
na mahitaji ya sasa.
Akifungua
kikao hicho Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto
Bibi Bibi Sihaba alisema kuwa ushiriki wa wadau kutoka ngazi ya
Halmashauri ni wa muhimu ili kuibua maoni ya wananchi yatakayosaidia
kuboresha sera iliyopo ili kuweza kuzingatia changamoto zinazowakabili
wanawake katika maeneo ya mijini na vijijini ili kufanikisha
azama ya Taifa ya kuwa na maendeleo endelevu kwa wanawake hapa nchini.
“Nyinyi
ni Wadau muhimu na ndio mnaosimamia utekelezaji wa Sera na mkikakati ya
Sera katika
ngazi ya mkoa na Halmashauri maoni na changamoto mnanazotukutana nazo ni
muhimu ili kujumuisha katika kipindi hiki cha kuhuisha Sera hii”
alisema Bibi Sihaba.
Akiongea
katika kuwasilisha mada elekezi, Mtaalamu Mwezeshaji Prof. Linda Mhando
amesema
Sera pendekezi itawezesha kufanya tathimi itakayotoa mwelekeo kuona kuwa
mipango na mkakati mbalimbali inazingatia mambo muhimu yanayohimiza
jamii kuachana na mitazamo ya kuwatambua wanawake peke yao, na badala
yake kutambua ushiriki wa wanaume kama wadau muhimu
katika Sera hii.
Pro
Linda, aliongeza kuwa Sera inayopendekezwa itahimiza ushiriki sawa wa
wanawake katika
ngazi za uongozi na maamuzi, upatikanaji wa haki sawa kwa wanawake,
uwepo wa hifadhi za jamii, kupunguza mzigo wa kazi, kuwashirikisha
wanawake katika shughuli za kiuchumi na kuwahusisha wanawake katika
fursa mbalimbali ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu.
Akizungumaza
katika kikao hicho Bi. Dafrosa Sanga Mchumi Wizara ya Maliasili na
Utalii alibainisha
kuwa sera hii iwanufaishe wavulana na wasichana, wanawake na wanaume
kwani hivi sasa watoto wengi wa kiume ndio wanaoathiriwa zaidi na utoro
shuleni na maisha ya mitaani ukilinganisha na watoto wa kike. Wadau
wameipongeza Wizara kwa uamauzi wake wa kuwashiriukisha
wadau wa ngazi zote ili kupanua wigo wa maoni katoka ngazi mbali mabli
kwa ajili ya umiliki wa sera hiyo na uzingatiaji wa haki kijinsia.
Maoni ya wadau yatakuwa msingi wa kuboresha Sera iliyopo ili kuimarisha uandaaji wa sera
inayokidhi upatikanaji wa haki za wanawake na wanaume katika ngazi mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment