Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akisisitiza jambo
alipokuwa akikagua mfumo wa kielektroniki katika Kituo cha Afya Makole
Manispaa ya Dodoma.
Wagonjwa wakiwa katika dirisha la malipo kwenye kituo cha Afya Makole Manispaa ya Dodoma.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akisalimia wagonjwa
alipokuwa akikagua kituo cha Afya Makole Manispaa ya Dodoma.
NAIBU
Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)
Selemani Jafo amefanya ziara leo ya kukagua utekeleza wa maagizo ya
serikali aliyoyatoa hivi karibuni katika Kituo cha Afya Makole Manispaa
ya Dodoma.
Pamoja na maagizo mengine, Jafo aliagiza kuhakikisha kituo hicho kinafunga mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji mapato.
Akiwa
katika ziara yake leo, Jafo amepongeza ufungaji wa mfumo huo huku
akiwataka kuhakikisha wanaziba mianya ya upotevu wa mapato kwa kuwa hali
ya ukusanyaji bado hairidhishi.
Amesema
kwa mujibu wa taarifa aliyoipata kituo hicho kabla ya mfumo kilikuwa
kikikusanya Sh.Milioni nne lakini kwasasa kinakusanya hadi Sh.Milioni
9.9 kwa mwezi jambo ambalo linaonesha bado kuna mianya ya upotevu wa
mapato.
“Nawapongeza
kwa kutekeleza maagizo ya serikali kwa kufunga huu mfumo lakini
sijaridhishwa na ukusanyaji mapato wa kiwango hichi, kuna vituo
vinakusanya hadi Sh.Milioni 24 nyie mnakusanya hivi bado haitoshi
hakikisheni mnaziba mianya,”amesema Jafo
Ameongeza
“Kuwepo na mfumo ni jambo moja na kuutumia mfumo ni jambo jingine jambo
la msingi ni uaminifu kuna watu katika vituo vyetu uaminifu ni mdogo
kwenye kukusanya fedha ndio ugomvi huwa unazuka na wakati mwingine watu
wanatolewa kwa maslahi yao binafsi,”.
Amewataka kuhakikisha kunakuwepo na matumizi sahihi ya mfumo huo ili kuongeza mapato.Akizungumzia
kuhusu ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya nchini, Jafo amesisitiza
Mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha zinasimamia kikamilifu ujenzi
huo na ifikapo Desemba 30 mwaka huu uwe umekamilika.
Amesema
hivi karibuni serikali imetoa Sh.Milioni 500 kwa kila kituo kimoja kwa
ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo jengo la
upasuaji,maabara ya kisasa na wodi ya akina mama na watoto.
Naibu
Waziri huyo amesema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk.John
Magufuli imedhamiria kuboresha huduma za afya na kwamba utoaji wa fedha
huo umetokana na hali ya vituo vya afya kuwa si ya kuridhisha.
Amebainisha
Dodoma ni eneo mkakati kutokana na wingi wa watu hivyo ni lazima huduma
za afya ziboreshwe ili kuondoa msongamano katika hospitali ya rufaa ya
Mkoa wa Dodoma.
Kwa
upande wake, Katibu wa Afya wa kituo hicho, Habiba Thabiti amesema kabla
ya kufungwa mfumo huo walikuwa wanakusanya Sh.Milioni nne kwa mwezi
lakini kwasasa wamefikia Sh.Milioni 9.9.
Naye,
Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk.George Matiko amesema kwa siku kituo
kinahudumia wagonjwa kati ya 400-800 na akina mama wanaojifungua kwa
mwezi ni 400.
0 comments:
Post a Comment