Home » » WAHARIRI NA WAANDISHI WA MAGAZETI MATATU WAHOJIWA MBELE YA KAMATI YA BUNGE YA MAADILI KWA KOSA LA KUTOA TAARIFA ZINAZOHUSU USHAHIDI NA MWENENDO WA KIKAO CHA KAMATI HIYO BILA KUPATA IDHINI YA BUNGE

WAHARIRI NA WAANDISHI WA MAGAZETI MATATU WAHOJIWA MBELE YA KAMATI YA BUNGE YA MAADILI KWA KOSA LA KUTOA TAARIFA ZINAZOHUSU USHAHIDI NA MWENENDO WA KIKAO CHA KAMATI HIYO BILA KUPATA IDHINI YA BUNGE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mtanzania Bw. Denis Msacky akijieleza mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Nipashe kwa kosa la kutoa taarifa zinazohusu ushahidi na mwenendo wa kikao cha Kamati hiyo bila kupata idhini ya Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 34 (1) (f) na (g) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.
Mhariri/Mwandishi wa Habari Gazeti la Mtanzania Bw. Bakari Kimwaga akiapaa kabla ya kuanza akijieleza mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Nipashe kwa kosa la kutoa taarifa zinazohusu ushahidi na mwenendo wa kikao cha Kamati hiyo bila kupata idhini ya Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 34 (1) (f) na (g) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi Bw. Angetile Osiah na Mwanasheria wake mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Nipashe kwa kosa la kutoa taarifa zinazohusu ushahidi na mwenendo wa kikao cha Kamati hiyo bila kupata idhini ya Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 34 (1) (f) na (g) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.
Mhariri wa Gazeti la Nipashe Bw. Edmond Msangi akijieleza mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Nipashe kwa kosa la kutoa taarifa zinazohusu ushahidi na mwenendo wa kikao cha Kamati hiyo bila kupata idhini ya Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 34 (1) (f) na (g) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.
PICHA NA OFISI YA BUNGE


Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imewahoji wahariri pamoja Waandishi wa Habari wa Magazeti ya Mtanzania, Mwananchi na Nipashe kwa kosa la kutoa taarifa zinazohusu ushahidi na mwenendo wa kikao cha Kamati hiyo bila kupata idhini ya Bunge.

Akizungumza mara baada ya kuwahoji mashahidi hao, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Almasi Athuman Maige (Mb) alisema wahusika wote walifika mbele ya Kamati na kujibu tuhuma hizo ambazo ni kinyume na kifungu cha 34 (1) (f) na (g) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.

Mheshimiwa Maige alisema Kamati baada ya kuwasikiliza mashahidi wote waliofika itaandaa Taarifa yake na kuiwasilisha kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai.“Kanuni zimeweka masharti kuwa shughuli za Kamati hii zinazofanywa zitabakia kuwa ni siri hadi hapo itakapomaliza kazi yake na kuwasilisha taarifa Bungeni,” alisema.

Aliwataja waliofika katika Kamati hiyo kuwa ni Ndugu Denis Msaki ambaye ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mtanzania na mwandishi wake Ndugu Bakari Kimwanga, Ndugu Edmond Msangi Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe na mwandishi wake Ndugu Gwamaka Alipipi na Ndugu Angetile Osiah Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi na Mwandishi wake Ndugu Elias Msuya.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa