Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe (kushoto) akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita na OCD - Gairo, Mratibu Mwandamizi Jeshi la Polisi, Ramadhani Kitantu (kulia) wakati alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi Idibo, shule ya sekondari ya kata ya Idibo sambamba na ugawaji wa mabati na vifaa mbali mbali kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Kituo cha Polisi Idibo.
Ukaguzi wa Ujenzi shule ya Sekondari Kata ya Idibo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe (wa kwanza kulia) akabidhi msaada wa mabati 120 na vifaa mbalimbali kwa Jeshi la Polisi na uongozi wa kata ya Idibo kwa ajili ya kupaua kituo cha Polisi Idibo kilichojengwa kwa nguvu za wananchi.
Wananchi na Wazee Maarufu wakifatilia mkutano na makabidhiano.
Mkuu
wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe ameagiza kukamatwa kwa
viongozi wote waliofuja shilingi milioni 32 za ujenzi wa shule ya
sekondari ya Kata ya Idibo.
Kauli
hiyo ameitoa leo wakati alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa shule hiyo
lililokwenda sambamba na ugawaji wa mabati na vifaa mbali mbali kwa
ajili ya kumalizia ujenzi wa Kituo cha Polisi Idibo.Mhe.
Mchembe aliwaomba TAKUKURU kuwakamata viongozi wote wanaosimamia ujenzi
wa shule ili waweze kuhojiwa matumizi ya pesa na wizi uliotokea tokea
kuanza kwa ujenzi huo.
"Nimepokea
taarifa ya Kamati ya Ujenzi ambayo imebaini wizi wa shilingi milioni 12
na matumizi ya utata yenye thamani ya shilingi milioni 20, hivyo
ninawaagiza TAKUKURU na OCD ndani ya siku saba kuwakamata wale wote
wanaohusika na sheria ichukue mkondo wake," alisema Mhe. Mchembe.
Aidha mpaka sasa japo kuna dosari Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata Idibo umemaliza madarasa 3, vyoo na jengo la utawala.Wakati
huo huo Mhe. Mchembe alikabidhi msaada wa mabati 120 na vifaa
mbalimbali kwa ajili ya kupanua kituo cha Polisi Idibo kilichojengwa kwa
nguvu za wananchi.
Katika
hafla hiyo, Mhe. Mchembe aliyepokelewa na mwenyeji wake OCD - Gairo,
Mratibu Mwandamizi Jeshi la Polisi, Ramadhani Kitantu, alitoa pongezi
kwa Diwani Kata ya Idibo Mhe. Rajabu Mguhi na viongozi wake wote na
wananchi wa Idibo kwa michango yao hadi boma kukamilika.
Mhe.
Mchenbe aliwaomba wananchi washiriki kuchangia awamu ya pili ya
umaliziaji bila kusahau nyumba za Polisi. Pia anakaribisha Wadau wengine
wa maendeleo wenye Mapenzi mema na Gairo TUSHIRIKIANE.
Katibu
Tawala Wilaya Bw. Adam John wakati wa ziara hizo alisisitiza wananchi
kushirikiana na Serikali ili kujiletea Maendeleo yao. Pale ambapo kuna
matatizo atahakikisha anayashughulikia ipasavyo kwa mujibu wa Sheria,
Taratibu na Kanuni (STK). Ndani ya mwaka mmoja tumefanikiwa kufungua
Sekondari za Kata mbili ambazo ni Chagongwe na Chanjale. Kote huko
watoto walikuwa wanatembea zaidi ya km 20 kwenda shule na maabara sita.
Miradi
yote ni nguvu za wananchi kwa zaidi ya asilimia 45 na fedha kutoka
Serikali. Pongezi kwa Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa
kuwajali watoto wa masikini huku pembezoni vijijini kabisa ambapo nao
wanajisikia vizuri na wanajenga Uzalendo wa kuipenda nchi yao tangu
wadogo.
Gairo
ina kituo kimoja tu cha Polisi hivyo hiki kitakuwa cha pili. Kituo hiki
kitahudumia Kata tano za Gairo na Kata jirani zaidi ya sita kutoka
Wilaya ya Kilindi, Kiteto na Mvomero kwani kipo mpakani mwa Wilaya hizo.
0 comments:
Post a Comment