NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, RUVU
KAMATI
ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, imeipongeza Mamlaka ya Maji Safi na
Maji Taka (DAWASA) na Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka, (DAWASCO), kwa
kazi nzuri ya usimamizi wa miradi ya uboreshaji wa huduma za ugawaji na
usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam na
Pwani.
Akizungumza
kwenye majumuisho ya ziara ya kamati hiyo baada ya kutembelea miradi
inayotekelezwa na kusimamiwa na DAWASA na DAWASCO Dar es Salaami na mkoa
wa Pwani leo Januari 20, 2018, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Mhe.Emmanuel Papian, alisema. Kazi iliyofanyika ni kubwa na Kamati
imeona jinsi gani fedha za serikali zimetumika.
Hata
hivyo Mwenyekiti huyo alisema, miradi mingi inatekelezwa kwa fedha za
mkopo kutoka India, lakini Kamati imebaini kuwa kila kitu kinafanywa na
makampuni ya kutoka India, jambo ambalo sio sahihi sana.“Inawezekana
kuna mahali ambapo tumezidiwa, au kujichanganya, na kama ni kwenye
component ya huo mkopo iliandikwa, kuna jambo la kuangalia na kujadili.”
Alisema Mhe. Papian.
Aidha
Mhe. Papian alisema Kamati inashauri kuwa watendaji wa ndani
(Wakandarasi) wanapomaliza hii miradi basi vijana wa Kitanzania lazima
wawe wameshajua na kufundishwa na wajifunze kila kitu ili waweze
kuendesha miradi hii kikamilifu.
Ziara
ya Kamati hiyo ilianzia makao makuu ya DAWASA, ambapo Kamati ilipokea
taarifa ya utendaji ya DAWASA na DAWASCO, na kasha walipata fursa ya
kutembeela baadhi ya miradi hiyo ambayo ni ujenzi wa matenki makubwa ya
kuhifadhia maji ya Changanyikeni, Salasala, vituo vya kusukuma maji vya
Makongo na Salasala.
Kamati
pia ilitembelea eneo la utandazaji mabomba ya kusambaza maji huko Mpiji
Machimbo na kumalizia ziara yao kwa kutembelea mitambo ya maji ya Ruvu
chini na Ruvu Juu.Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo, Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangi’ngo alisema,
Mradi wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika
baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani unaendelea kwa kasi
katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na katika Miji ya Bagamoyo
na Kibaha na tayari umefikia asilimia 72.2 kukamilika.
“Mradi
huu unatekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya
Maji Safi na Maji Taka, (DAWASA), ulianza rasmi Machi mwaka 2016 na
unatarajiwa kukamilika Februari 28, 2018.” Alisema.Akifafanua zaidi
kuhusu kazi zinazofanyika kwa sasa, Mhandisi Mwang’ingo alitaja kuwa ni
pamoja na ujenzi wa matenki tisa (9) ya kuhifadhi na kusambaza maji
yenye ukubwa wa kuhifadhi kati ya lita za ujazo milioni 3.0 hadi milioni
6.0 ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vine vya kusukuma maji na
ununuzi na ufungaji wa pampu kubwa za kusukuma maji 16.
Kazi
nyingine ni pamoja na ununuzi wa transfoma na ufungaji njia za umeme wa
msongo mkubwa, ununuzi na ulazaji mabomba yatakayokuwa na urefu wa jumla
ya kilomita zipatazo 477.“Maeneo yatakayofaidika na mradi huu ni pamoja
na Salasala, Bunju, Wazo, Makongo, Changanyikeni, Bagamoyo, Mpiji,
Zinga, Kiromo, Kitopeni, Ukuni, Buma, Mataya na ukanda maalum wa WPZA
ambayo ni maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu Juu.” Alifafanua.
Aidha
maeneo mengine yatakayofaidika na mradi huu ni pamoja na Mbezi Louis,
Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Msakuzi, Makabe, Malamba Mawili na Msigani na
maeneo hayo yote yanapata huduma ya maji kutoka mtambo wa Ruvu Juu
uliozindulkiwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli Juni 21, 2017.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA, Bw.;aston T.
Msongole, alisema ni nia ya DAWASA kuhakikisha maeneo yote ambayo
hayajafikiwa na huduma ya maji hususan baadhi ya maeneo ya wilaya mpya
ya Kigamboni, ni kuhakikisha huduma hiyo inawafikia.
“Tayari
tumechimba visima virefu vyenye uwezo wa kutoa maji mengi ya kumaliza
tatizo la ukosefu wa maji kwenye maeneo hayo lakini tatizo ni uhaba wa
fedha za kutengeneza mfumo wa kuyasambaza maji hayo kwa walaji” Alisema
Bw.Msongole.
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangi’ngo(kushoto),
akifafanua jamnbo mbele ya Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji,
Mifugo na Kilimo, Mhe. Emmanuel Papian, (Kulia) na baadhi ya wajumbe wa
kamati hiyo, walipotembelea ujemnzi wa tenki la kuhifadhia na kusambaza
maji la Salasala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam leo Januari 20,
2018.
Mjumbe
wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Daniel;
Nsanzugwanko, (katikati) akizunguzma jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa
DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangi’ngo, (kushoto) na Kaimu Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Emmanuel Papian,
walipotembelea mtambo wa maji wa Ruvu Juu, Mlandizi mkoani Pwani.
Kaimu
Mwewnyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji, Mifugo na Kilimo, Mhe. Emmanuel
Papian, (Kushoto) na mjumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Daniel Nsanzugwanko,
(katikati), wakimsikilzia Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS
limited ya India, wakati wa ziara ya Kamati hiyo kwenye eneo la ujenzi
wa mtambo wa kusukuma maji wa Salasala.
Taswira
ya maendeleo ya ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhi na kusambaza maji la
Salasala ukiwa umefikia hatua ya ufunikaji kabla ya kumwaga zege.
Mafundi wakisuka non do tayari kwa kumwaga zege kwenye tenki la Salasala.
Modester
Mushi (kushoto), ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa ufundi DAWASA akiwa na
Afisa Habari na UHusiano wa Jamii Mwandamizi wa Mamlaka hiyo, Bi.Mecky
Mdaku wakati wa ziara hiyo ya Kamati ya Bunge huko Salasala.
Kaimu
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Emmanuel Papian, (kushoto), akizungumza
jambo na Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, Bi. Neli Msuya.
Kamati ikipokea taarifa ya utendaji ya DAWASA/DAWASCO mwanzoni mwa ziara hiyo.
Meneja Uhusiano wa Jamii, DAWASA, Bi. Neli Msuya, akigawa taarifa ya DAWASA kwa wajumbe wa Kamati.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati, wakisikiliza taarifa hiyo.
Mjumbe wa Kamati, Mhe,Kuntyi Yusuph Majala, akizunhgumza wakati wa Kamati ikipkea taarifa.
Mhandisi Mwangi’ngo, akitoa taarifa ya utendaji ya DAWASA.
Picha ya pamoja ya Kamati na watendaji wa DAWASA/DAWASCO na wajenzi.
Sehemu ya mtambo wa maji Ruvu Chini.
Sehemu ya mtambo wa maji Ruvu Chini.
0 comments:
Post a Comment