Spika
wa Bunge Job Ndugai amefunguka na kusema Mbunge wa Singida Mashariki,
Tundu Lissu pamoja na familia yake hawatambui kuwa Serikali hasa Bunge
limeanza kufanya mazungumzo na watu wanaotaka kumsafirisha kwenda nje
kwa matibabu zaidi.
Ndugai
amedai anatambua kuwa Tundu Lissu atasafirishwa na kwenda kwa matibabu
zaidi nje ya Kenya ingawa hajajua ni lini lakini amesema kuwa watu ambao
wamepanga kumpeleka huko kwenye matibabu tayari walishamtafuta yeye na
kusema watashirikiana nao katika masuala ya matibabu.
"Ni
kweli kwamba atapelekwa nje zaidi ya Nairobi ila bado sijui mpaka sasa
ni lini kwa kuwa sijajua tarehe bado japo nadhani itakuwa hivi karibuni
na wale wanaomgharamia kumpeleka nje wameshawasiliana na mimi na hakika
familia ya Lissu hata Tundu Lissu mwenyewe hajui hilo, anafikiri ni wao
peke yao lakini najua na walishafika kwangu na kusema watagharamia wao"
alisema Ndugai
Spika
Ndugai alizidi kueleza kuwa endapo watakubaliana na watu hao basi wao
kama Serikali watagharamia katika mambo mengine ambayo yatawashinda hao
wadau ambao walimfuata na kuongea naye.
"Gharama
ambazo sisi tunaweza kuziingia endapo tutakubaliana na maamuzi hayo
kufanyika itakuwa katika yale mambo mengine yanayobakia ambao wale kama
wadau, wawezeshaji, wanaotusaidia hawataweza kutoa na ili liafikiwe
lazima tuwe na uhakika kitu gani kinalipiwa na kitu gani hakilipiwi
vinginevyo tutalipa mara mbili mbili sisi tunalipa wenzetu wanalipa
ambapo kidogo italeta mchanganyiko usiokua na afya" alisisitiza Ndugai
Mwaka
jana Tundu Lissu alidai kuwa Serikali pamoja na Bunge bado walikuwa
hajachangia jambo lolote katika matibabu yake ambayo yanaendelea mpaka
sasa nchini Kenya jijini Nairobi kufuatia shambulio lake la kupigwa
risasi Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment