Mkuu wa Wilaya ya Kondoa ( wa tatu kushoto waliosimama) akiwa katika ya pamoja na wajumbe wa bodi ya afya Kondoa Mji na sekretarieti wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mh. Sezaria Makota (wa tatu kushoto) akimkabidhi kitendeakazi mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Afya Halmashauri ya Mji Kondoa wakati wa uzinduzi wa wa bodi hiyo hivi karibuni.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mji Kondoa akitoa mafunzo kwa wajumbe wapya wa Bodi ya Afya ya Mji wa Kondoa.
Mkuu
wa Wilaya ya Kondoa Mh. Sezaria Makota amewataka wajumbe wa bodi ya
Afya Kondoa Mji kutekeleza majikumu yao kwa umakini na weledi ili
kuhakikisha kuwa huduma za Afya zinaimarika.
Aliyasema
hayo wakati wa uzinduzi wa bodi ya Afya uliofanyika katika ukumbi wa
jengo la Biashara Kondoa ikiwa ni bodi ya kwanza tangu kugawanywa kwa
Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na kupatikana kwa Halmashauri ya Mji.
“Kwasasa
usimamizi wa Hospitali ya Wilaya utakuwa chini ya Halmashauri ya Mji
Kondoa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa hivyo ni jukumu lenu
kuhakikisha hospitali inakua.”alisema Makota
Aliongeza kuwa kwasasa halmashauri haina vituo vya Afya na Zahanati ni chache hivyo
ni jukumu lao kuhakikisha vyote vinaanzishwa na kuongezeka ikiwa ni
pamoja na kuongeza mapato ya Hospitali na zahanati kwa ajili ya
kuboresha miundombinu yake.
Aidha
akiongea katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa
Mh. Hamza Mafita alisema kuwa wajumbe waliochaguliwa ndio watendaji
wakuu wa mabadiliko ya huduma ya Afya hivyo watakutana na changamoto
nyingi na wanapaswa kuzitatua na kuzipeleka mbele watakazoshindwa
kuzitatua ili washirikiane kuzitatua.
Bodi
ya Afya ya Halmashauri ya Mji Kondoa imezinduliwa kwa mara ya kwanza
kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ambapo Dkt. Maulid Majala
alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi, Emiliana Komolo Makamu Mwenyekiti
na Dkt. Eusebi Kessy kuwa Katibu wa Bodi.
0 comments:
Post a Comment