WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inataka kuimarisha masoko ya
mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kupata tija.
Aliyasema
hayo jana (Februari 2, 2018) wakati akikagua Kampuni ya Soko la Bidhaa
Tanzania (TMX), iliyoanzishwa kwa lengo la kuimarisha masoko.
Alisema
kupitia Wizara ya Kilimo, Serikali imedhamiria kuimarisha masoko ya
mazao yanayolimwa nchini ili kuwawezesha wakulima kujikwamua kiuchumi.
“Kupitia
Wizara ya Kilimo tunataka kuimarisha masoko ya mazao yanayolimwa
nchini. Wakati umefika kwa wakulima nchini kuona tija ya mazao
wanayolima.”
Alitoa
mfano wa zao la pamba ambalo wakulima walikuwa wanaingia mikataba na
wanunuzi, mfumo ambao ulikuwa unawanyonya badala ya kuwanufaisha.
Awali,
Afisa Mtendaji Mkuu wa TMX, Bw. Godfrey Malekano alimuhakikishia Waziri
Mkuu kwamba wamejipanga vyema kuanza minada ya mazao.
“Tutaanzia na zao la ufuta mwezi Mei 2018 na kuendelea na mazao mengine kwa kadiri ya misimu ya mazao hayo ilivyo.”
Alisema
kufanikiwa kwa Soko la Bidhaa na Mfumo wa stakabadhi ghalani
kunategemea sana msaada wa Serikali. “Soko la Bidhaa la Ethiopia
linalotajwa sana kwa mafanikio, limefikia malengo yake kutokana na mkono
wa Serikali.”
Bw.
Malekano alisema kutokana na umadhubuti wa Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli wanamatumaini makubwa kwamba
soko hilo litatimiza malengo yake.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMAMOSI, FEBRUARI 3, 2018.
0 comments:
Post a Comment