Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna
Tarishi (katikati) akisisitiza jambo wakati akifungua Kikao cha Baraza
la wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu lililofanyika tarehe 21Machi,
2018 mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna
Tarishi akiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano pamoja na wajumbe wa Baraza
la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo mjini Dodoma kabla ya kufungua Kikao
hicho.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiimba
wimbo wa Umoja na Mshikamano leo mjini Dodoma kabla ya kufunguliwa kwa
Kikao cha baraza hilo .
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu
Bi. Maimuna Tarishi ameongoza Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi
hiyo na kuwaasa wajumbe wa baraza kutoa maoni yatakayosaidia kufanikisha
mchakato wa maandalizi ya Bajeti ya mwaka 2018/2019.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao hicho Tarishi amesema kuwa Watumishi wote katika Ofisi hiyo wanao wajibu wakushiriki kikamilifu katika mchakato wa maandalizi ya bajeti ili kufanikisha azma ya Serikali kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
“Bila kujali nafasi zenu ni lazima mtambue kuwa mnao wajibu sawa katika kutoa maoni yatakayosaidia katika mchakato wa maandalizi ya bajeti” alisisitiza Bi. Tarishi.

0 comments:
Post a Comment