Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (wa kwanza kulia) na wageni wake kutoka Sweden wakishiriki msaragambo na wanawake wa Kata ya Chakwale kuchimba mtaro wa kutandaza mabomba ya Maji.
Mhandisi Magumbo (wa kwanza kushoto) anayekuwa akisimamia mradi huo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Mchembe (katikati) na wafadhili kutoka nchini Sweden mara baada ya kufika kukagua.
Mhandisi wa Wilaya ya Gairo Heke Bulugu akitoa ufafanuzi kwenye baadhi ya mambo.
Akitembelea mradi Maji Safi na Salama uliopo Gairo, Mkuu wa Wilaya
ya Gairo, Mhe. Mchembe akiwa ameongozana na Mhandisi wa Maji Wilaya
Eng. Heke Bulugu, Madiwani wa Chakwale na Madege pamoja na Watendaji
wao, na Mhandisi wa Lions Pure Water Eng. Magumbo pamoja na wafadhili wa
kutoka nchini Sweden; Mhe. Mchembe ameeleza kuwa Mradi huo unahudumia
kata 2 za Madege na Chakwale na vijiji 6 vya Madege, Ng'olong'o ,
Sanganjelu, Chakwale, Kilimani na Kimashale.
Aliongeza kuwa utanufaisha jumla ya wananchi 10,358 kwa gharama ya
shs 348,000,000/- kwa mchanganuo ufuatao Lions Pure Water shs
278,000,000/- Halmashauri kupitia Serikali kuu shs 48,000,000/- na Nguvu
za wananchi 22,000,000/-
Mhe. Mchembe ameisifia serikali ya Rais Dkt. Magufuli ya hapa Kazi
tu! kwa kuweza kuwajali wanyonge kwa kuwatua ndoo kichwani akinamama.
0 comments:
Post a Comment