Home » » UPINZANI:MSIKUBALI CCM IWABURUZE KATIBA MPYA

UPINZANI:MSIKUBALI CCM IWABURUZE KATIBA MPYA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Katibu Mkuu wa Chadema,Willibrod Slaa.
 
Vyama  vya vitatu vya upinzani, vimewataka wananchi kutokubali kuburuzwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mchakato wa Katiba mpya.
Kauli hiyo ilitolewa na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi katika mkutano wa hadhara wa pamoja kuzungumzia Rasimu ya  Katiba mpya.

Mkutano huo ulifanyika katika uwanja wa Ng'ombe wilayani Muheza na kuhudhuriwa na watu wengi.

Katibu  Mkuu wa Chadema, Willibrod Slaa, aliwataka wananchi kutokubali kuburuzwa katika majadiliano ya mchakato wa Rasimu ya Katiba mpya na CCM.

Dk. Slaa alisema hata wabunge wa upinzani bungeni walikataa kuburuzwa na ndiyo maana mchakato wa Katiba ukafikia hapa ulipo.

Alifafanua kuwa wabunge wa upinzani walikuwa wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge wanapoona kanuni zinapindishwa.

Alisema kuwa CCM haitaki serikali tatu na kwa maana hiyo itawabana wananchi wakubaliane na hilo.

Dk. Slaa aliwataka vijana kukomaa na kuhakikisha kwamba wanalikataa hilo.

Alisema kuwa CCM haitaki maoni ya Tume ya Jaji mstaafu Joseph Warioba, kwa kuwa ni yana ukweli ndani yake kwa kupendekeza muundo wa serikali tatu.

Hata hivyo, alisema kuwa wajumbe 600 wa Bunge la Katiba waliopo bungeni, hawawezi kuwashinda wananchi katika mchakato wa kupitisha muundo wa serikali tatu.

Dk. Slaa aliwataka wanachi kukubali mfumo wa serikali tatu kwa maelezo kwamba ndiyo mkombozi wao katika maendeleo na kuwadhibiti mafisadi.

Kwa upande wao, Kaimu Katibu Mkuu wa CUF Taifa, Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa Usalama Chadema, Wilfred Lwakatare, Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Musane Yambabe na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CUF Taifa, Nuru Awadh, kwa nyakati tofauti, waliwataka wananchi kuhakikisha wanapendekeza muundo wa serikali tatu.

Viongozi hao walisema katika kipindi cha miaka mingi, wananchi `wamepigika' sana katika nyanja mblaimbali ikiwamo elimu na afya na kwamba muundo wa serikali tatu ndiyo itakayotatua matatizo yao.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa