Home » » SALMA:SURA YA KWANZA NA SITA ZITAZUA MJADALA MKALI

SALMA:SURA YA KWANZA NA SITA ZITAZUA MJADALA MKALI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba
 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Salma Said, amesema mjadala wa sura ya kwanza na ya sita ya Rasimu ya Katiba unaotarajiwa kuanza leo utakuwa mkali.

Salma ambaye anatoka kundi la wajumbe wa kuteuliwa 201, aliliambia gazeti hili kuwa hali hiyo inatokana na mvutano ulioonekana wakati wa uwasilishaji wa taarifa za kamati zilizokuwa zinachambua sura ya kwanza inayozungumzia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya sita inayozungumzia muundo wa Muungano na kutoa mapendekezo kuanzia Alhamisi hadi Jumamosi.

Kamati 10 kati ya 12 ziliwasilisha taarifa zao bungeni na leo kamati mbili zilizobakia Namba 6 na 7 zitamalizia kisha kufuatiwa na mjadala wa sura hizo.

“Hakuna mwelekeo mzuri wa Katiba zaidi ya mabishano, wajumbe hatujajenga hoja zaidi ya misimamo,” alisema Salma, ambaye ni mwandishi wa habari kitaaluma.

Aliongeza: “Mjadala utakwenda kimisimamo kwa sababu hatutaki kulegeza na kusimamia katika hoja.”

Kwa mujibu wa Salma, matatizo yanayotokea katika bunge hilo yanatokana na kuingizwa wanasiasa wengi, wangetafutwa watu neutral (wasioegemea upande wowote) mambo yangekwenda vizuri.

Alisema anawashangaa wajumbe wanaosema kwamba bila serikali mbili Muungano utavunjika wakati wananchi wa pande zote walikuwa na udugu kabla ya Muungano huo mwaka 1964.

Alisema pamoja na tofauti za kimisimamo, wananchi watatoa maamuzi ya kweli kwa kuwa hivi sasa wamepata mwekeleo kupitia vyombo vya habari.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa