Home » » WAZIRI MKUU AHIMIZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

WAZIRI MKUU AHIMIZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Imeandikwa na Katuma Masamba, Dodoma
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifunga Bunge jana mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema, serikali imeandaaa mikakti mbalimbali ya kudhibiti na kukabiliana na changamoto ya uharibifu wa mazingira, hususan uharibifu wa vyanzo vya maji, matumizi yasiyo endelevu ya ya ardhi, misitu na bioanuai nyingine.

Waziri Majaliwa ameyasema hayo wakati wa kuahirisha mkutano wa Bunge, mjini Dodoma ambapo amesema, mikakati hiyo ambayo inatekelezwa na sekta zote ni pamoja na Mkakati wa Taifa wa kukabliana na Mabadliko ya Tabia Nchi, Mkakati wa Taifa wa hatua za haraka za kuhifadhi mazingira ya pwani, bahari, mito na mabwawa.

“Mikakat mingine ni Mkakati wa Taifa wa kupanda na kutunza miti, Mkakati na Mpango kazi wa Taifa wa Hfadhi ya Bioanuai na Programu ya kukabiliana na kuenea kwa hai ya jangwa na ukame,” amesema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu ameahrisha Bunge hadi Januari 30, mwakani .
CHANZO HABARI LEO 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa