Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bubutelo wilayani Chemba.
Mbunge wa Chemba Juma Nkamia akizungumza na wananchi wa Bubutelo katika ziara ya Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso.
Wananchi wa Bubutelo wilayani Chemba wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso.
Naibu
waziri wa maji na umwagiliaji Jumaa Aweso amewataka wakandarasi nchini
kuwa wazalendo katika kuhakikisha fedha zinazopelekwa kwa ajili ya
kutekeleza miradi ya maji zinafanya kazi iliyokusudiwa.
Aweso
ametoa rai hiyo akiwa katika kijiji cha Bubutelo wilayani Chemba akiwa
katika ziara yake ya kutembelea na kuzumgumza na wananchi wa vijiji vya
Mombose na Bubutelo ambavyo vipo katika eneo linalotarajiwa kujengwa
bwawa la Farkwa.
Aweso
amesema serikali inajitahidi kutenga fedha ili kukamilisha miradi hiyo
na hatimaye ifikie azma ya kumtua ndoo ya maji kichwani kama
ilivyokusudiwa hivyo ni wajibu wao kuwa wazalendo.
"Mkandarasi
anayepewa kazi ajione kabisa yeye ni Mtanzania avae uzalendo kwa Taifa
lake,serikali inatenga fedha nyingi za miradi lakini wapo wakandarasi
ambao sio waaminifu jambo ambalo linakwamisha nia nzuri ya serikali
iliyonayo,"amesema Aweso.Katika
ziara hiyo Aweso amesikiliza vilio vya wananchi ambao wengi waliomba
kujua hatma ya fidia zao ili wapishe mradi huo suala ambalo amesema
linashughulikiwa na likikamilika kila anayestahili kulipwa atalipwa.
Kwa
upande wake mbunge wa Chemba Juma Nkamia amesema wananchi wameupokea
mradi huo vizuri na wanachosubiri ni fidia zao na kuwasisitiza wananchi
kuwapuuza baadhi ya watu wanaopita na kusema mradi huo haufai.Naye
kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Jofrey Pima amesema hali ya
upatikanaji wa maji ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya watu waliokuwepo
ambapo mijini wananchi 4490 ndio wanapata maji na kijijini ni asilimia
44.
"Bwawa
la Farkwa likikamilika litasaidia kuongeza idadi ya wanaopata maji na
hivyo kukidhi dhamira ya serikali,kwa sasa upembuzi yakinifu
umeshafanyika,tunasubiri suala la kuwalipa fidia wananchi,"amesema kaimu
mkurugenzi huyo.Wilaya
ya Chemba ilianzishwa mwaka 2012 na mwaka 2013 iliundwa halmashauri
ambapo ina jumla ya tarafa 4,kata 26 na vijiji 114 ikiwa na jumla ya
wakazi laki 256,623 kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment