Home » » HOJA YA MH. ZITTO KABWE YA KUPIGA KURA ZA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU YAPIGWA CHINI NA KANUNI ZA BUNGE

HOJA YA MH. ZITTO KABWE YA KUPIGA KURA ZA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU YAPIGWA CHINI NA KANUNI ZA BUNGE




Taarifa za hivi punde kutoka Bungeni Mjini Dodoma,zinaeleza kuwa
Kusudio la Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe la kutaka
kupiga kura za kuanzishwa kwa mjadala wa kutokuwa na imani na Waziri
Mkuu,Mh. Mizengo Pinda,limepigwa chini na Spika wa Bunge,Mh. Anne
Makinda.


Akisoma
kanuni za Bunge,Mh. Spika alisema kwa mujibu wa kanuni za Bunge na
Katiba ya Nchi,kusudio la kutaka kumuondoa Madarakani Waziri Mkuu kwa
kupiga kura ya kutokuwa na Imani nae ambayo ni taarifa ya maandishi
inapaswa kuwasilishwa kwake siku 14 kabla ya siku husika.


Hivyo
kwakuwa ofisi yake haijapata taarifa ya maandishi ju ya zoezi hilo,basi
zoezi hilo moja kwa moja litakuwa ni batili, na kwasababu kikao hicho
cha Bunge kinatarajiwa kufungwa siku ya jumatatu,basi hakutakuwa na
uwezekano wa zoezi hilo kukamilika.


Awali
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli,Mh. January Makamab aliomba muongozo wa
Spika kuhusu jambo hilo ndipo Spika,Mh. Anne Makinda akasimama na kutoa
ufafanuzi huo.
Na www.issamichuzi.blogspot.com 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa