Home » » WENYEVITI WA KAMATI ZA BUNGE ZA FEDHA ZA UMMA WAKUTANA NA KATIBU MKUU KIONGOZI, BUNGENI DODOMA

WENYEVITI WA KAMATI ZA BUNGE ZA FEDHA ZA UMMA WAKUTANA NA KATIBU MKUU KIONGOZI, BUNGENI DODOMA




Katibu Mkuu kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (Kulia) akimsikiliza mwenyekiti
wa kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. John Cheyo (katikati) wakati
alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa
kamati hiyo Mhe. Zainabu Vulu. Balozi Sefue alifanya ziara ya kikazi Bungeni
kwa lengo la kujitambulisha.



 Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Kulia) akimsikiliza makamu
mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) Mhe. Deo
Filikunjombe wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma. Katikati ni
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Zitto Kabwe. Balozi Sefue, alifanya ziara ya
kikazi Bungeni kwa lengo la kujitambulisha



 Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Kulia) akizungumza na
mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Mhe. Agustino Mrema
wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti
wa kamati hiyo Mhe. Idd Azzan. Balozi Sefue alifanya ziara ya kikazi Bungeni
kwa lengo la kujitambulisha.




Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akimkabidhi Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue, vitabu vya orodha ya Wabunge pamoja na kanuni za kudumu za
Bunge wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma, leo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa