Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisoma malezo ya awali kwa waheshimiwa wabunge namna ambavyo uchaguzi huo ulivyotakiwa kuendeshwa na taratibu zitakazofuatwa.ambapo uchaguzi ulifanyika na Wabunge tisa walipatikana watakaowakilisha nchi yetu kwenye Bunge la Afrika Mashariki ambao ni Bi. Angela Kizigha, Bi. Shy-Rose Bhanji,Bw. Mwinyi Hassan, Bw. Yahya Ussi, Bw. Taslim Issa,Bw. Kesi Papetua,Adam Kimbisa, Bernard Murunya na Makongoro Nyerere.
Zoezi la Uchaguzi likiwa linaendelea.
Mgombea Ubunge wa Afrika Mashariki katika Kundi la wanawake Bi. Shyroze Bhanji akijinadi kwa wabunge wakati wa zoezi la uchaguzi lililofanyika jana Bungeni Dodoma.
Naibu waziri wa Ujenzi Mhe. Harison Mwakyembe akimuuliza swali mmoja wa wagombea wa Bunge la Afrika Mashariki.
Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nassari akimuuliza swali mmoja wa wagombea wa Bunge la Afrika Mashariki.
Mgombea Ubunge wa Afrika Mashariki katika Kundi la Upinzani John lifa chipaka wa TADEA akijibu mojawapo ya maswali yalikuwa yanaulizwa na wabunge wakati wa zoezi la uchaguzi lililofanyika jana Bungeni Dodoma.
katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akitoa maelezo ya mwisho kwa wagombea wa Bunge la Afrika Mashariki kabla ya kuanza kwa zoezi la kujinadi Bungeni jana. kulia kwake ni Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge Nd. John Joel.
Picha zote na Issa Michuzi Blog
Picha zote na Issa Michuzi Blog
0 comments:
Post a Comment