Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli.
Habari tulizozipata punde zinadai kuwa Waziri wa Ujenzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amezidiwa ghafla na kukimbizwa hospitalini huku Dodoma ambapo bunge la tisa linaendelea.
Kwa mujibu wa Naibu Spika, Job Ndugai Dk. Magufuli alikumbwa na homa ya ghafla ambapo baada ya kukimbizwa General Hospital, Dodoma, ilibainika kuwa presha yake ilikuwa juu na ana kichomi upande wa kushoto wa mbavu zake.
0 comments:
Post a Comment