Sehemu ya Meza Kuu,Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama ambao ndio waandaaji wa tamasha la pasaka,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,Mh Betty Mkwasa,Naibu Spika wa Bunge,Mh. Job Ndugai pamoja na mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dr Rehema Nchimbi.
Muimbaji mahiri wa nyimbo za kusifu na kuabudu,Upendo Nkone akitumbuiza mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Dodoma waliojitokeza kwenye tamasha la jumatatu ya pasaka jioni ya leo.
Mmoja wa Waimbaji kutoka nchini Kenya,akitumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Pasaka ndani ya Uwanja wa jamhuri,mjini Dodoma
Malkia wa nyimbo za injili hapa nchini,Rose Muhando akiimba mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Dodoma waliojitokeza jioni ya leo kwenye tamasha la jumatatu ya pasaka
Pichani shoto ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr.Rehema Nchimbi akiwa na mkuu wa wilaya ya Dodoma,Betty Mkwasa wakiburudika kwa nyimbo za kiroho ndani ya uwanja wa jamhuri jioni ya leo,ambapo katika tamasha hilo mgeni rasmi ni Naibu Spika wa Bunge,Mh. Job Ndungai.
kwa mapicha zaidi ingia hapa JIACHIE BLOG
0 comments:
Post a Comment