Home » » WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WATEMBELEA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) JANA

WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WATEMBELEA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) JANA

 Kaimu  Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Mipango, Utawala na Fedha,Prof Shaban Mlacha (Katikati) Akitoa Maelezo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya waliotembelea Chuo hicho leo na kupata fursa ya kuona Maonyesho yaliyohusisha wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma.
Mmoja wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) akitoa maelezo kwa baadhi  ya wakuu wa wilaya na mikoa waliokuja Kuona kazi za wanafunzi wa UDOM wakati wanafunzi hao Wakionyesha Uwezo tofauti na Masomo wanayosomea.
Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakitembelea Jengo la Utawala la Chuo Kikuu Cha Dodoma na kufanya ziara ndani ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakati walipofika chuoni hapo Kuangalia maonyesho ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma yaliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu Cha Dodoma.
Baadhi ya Michoro iliyochorwa na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) ambazo leo wamepata nafasi ya kuonyesha kazi zao tofauti na masomo wanayosomea.
 Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakiwa katika Picha ya Pamoja Mbele ya Jengo la Utawala Mpya wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM).
Picha zote na Josephat Lukaza Blog

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa