Home » » JESHI LA POLISI DODOMA LAWAKAMATA WAGANGA WA KIENYEJI‏

JESHI LA POLISI DODOMA LAWAKAMATA WAGANGA WA KIENYEJI‏

Kiongozi wa kundi la waganga wa kienyeji maarufu kama Lambalamba
Majuto Muhamedi akielezea jinsi wanavyofanya kazi ya kutoa uchawi
kwenye nyumba mbalimbali mbele ya waandishi wa habari baada ya
kukamatwa na jeshi la Polisi mkoani Dodoma kutokana na kufanya
shughuli hizo ambapo kundi hilo ni mchanganyiko wa waganya kutoka
mikoa Tanga,Morogoro,Mtwara na Pwani,Picha na Masoud Masasi


Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma Zelothe Stephen akiwaonyesha waandishi
wa habari kifaa kinachojulikana kama sitemila ambacho utumiwa na
kundi la waganga wakienyeji maarufu kama Lambalamba kwa kushughuli zao
za kuwakamata wachawi ambapo jeshi hilo limewakamata waganga hao saba
kutokana na kuendesha shughuli hizo ambazo zimekuwa zikileta ufunjifu
wa amani kwa wananchi kutokana na imani za kishirikina,kulia kwake ni
kiongozi wa kundi hilo Majuto Muhamedi Picha na Masoud Masasi.

**********************
Masoud Masasi,Dodoma yetu
JESHI la Polisi mkoani Dodoma linawashikiria watu tisa wanaodaiwa kuwa
ni waganga wa kienyeji maarufu kama Lambalamba ambao wamekuwa
wakiwalaghai wananchi kwa kufanya shughuli za kutoa watu uchawi na
kusababisha kuwepo kwa uvunjifu wa amani.
Pamoja na kukamatwa kwa watu hao Jeshi hilo mkoani hapa limepiga
marufuku shughuli zote za uganga wa kienyeji ambapo wameunda kikosi
maalumu cha kufanya operesheni mkoa mzima.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa kamanda wa Polisi
mkoa wa Dodoma Zelothe Stephen alisema kundi hilo la matapeli wamekuwa
wakijishughulisha na shughuli za kitapeli kwa kujifanya waganga wa
kienyeji kinyume na sheria ya nchi.
Aliwataja waganga hao waliokamatwa kuwa ni Musa Omari(19) Abdallah
Musa wote ni wakazi wa mkoa ni Mtwara,Ally Shante(30) mkazi wa Kibaha,
Shabani Ramadhani(32) na majuto Mohamedi (32)kutoka Morogoro,Abdalah
Musa(16) na salehe Omari(26) na Mkude Mwenda na Joseph John wote
kutoka Tanga
Zelothe alisema watu hao ambao wanajulikana kwa jina la lambalamba
walikuwa wakifanya utapeli huo katika wilaya ya Kongwa kwa kuwatoa
uchawi watu mbalimbali jambo alilosema limekuwa likichochea chuki na
uadui kwa wananchi.
Alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunatokana na operesheni
iliyofanya na jeshi hilo kutokana na watu hao kufanya shughuli hizo
ambazo zimekuwa zikihatarisha amani kwa kuwagombanisha wananchi.
Alibainisha kuwa hivi karibuni kundi hilo lilileta vurugu baada ya
kutokea kwa kifo cha Martha Mapuga(34)mkazi wa kijiji cha Mlanje baada
ya baba yake Meshack Mapugakuwakatalia waganga hao kufanya shughuli
hizo nyumbani kwake.
Alisema baada ya waganga hao kuondoka ndipo Martha aliugua ghafla
alianza kuumwa tumbo ambapo alifariki wakati akiwa katika hospitali
ya wilaya ya Kongwa.
“Kutokana na sintofahamu ya wanakijiji hao walianza kuwatilia mashaka
kikundi hicho cha lambalamba hao walihusika na tukio hilo ndipo ndipo
walipojikusanya wakiwa na silaha za jadi kwa lengo la kutaka kuwaua
lakini walifanikiwa kuvunja mlango na kutoroka ”alisema Zelothe.
Kamanda huyo alisema kundi hilo limekuwa likisababisha watu kuuwawa na
wengine kuchomewa nyumba zao kutokana na kuwataja watu wachawi ambao
wamekuwa wakiroga watu mbalimbali.
Alisema kuanzia sasa jeshi hilo limepiga marufuku shughuli zote za
uganga wa kienyeji ambapo amesema wameunda kikosi maalumu ambacho
kitakuwa kikifanya operesheni ya kuwakamata watu wote
wanaojishughulisha na shughuli hizo.
“Kuanzia sasa sitaki kuona wala kusikia sijui mganga katoka sumbawanga
wala wapi tumeunda kikosi maalumu kwa ajili ya kushughulika nao na pia
wananchi muwe mnatupa taarifa za hawa watu na sisi tutawakamata kwa
kuwa wanachokifanya ni uvunjifu wa amani”alisema Kamanda huyo.
Kwa upande wao mmoja wa waganga hao waliokamatwa Majuto Muhamedi
alisema wamekuwa wakifanya shughuli hizo za kutoa uchawi sehemu
mbalimbali hapa nchini kwa mwaliko maalumu wa viongozi wa vijini na
kata.
“Kama kuna tatizo eneo husika la kuwepo kwa vitu kama pembe,mizukule
na mtu ambaye anafahamika kwa uchawi basi huwa tunaitwa kwa mwaliko
maalumu kutoka kwa viongozi wa kijiji na sisi tunakwenda kufanya kazi
hiyo na wakati mwingine tunatoa hadi fisi na nyoka kwenye nyumba
mbalimbali”alisema Mohamedi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa