Home » » SERIKALI YATAKIWA KULIPA DENI LA BIL 41 LA MSD‏

SERIKALI YATAKIWA KULIPA DENI LA BIL 41 LA MSD‏

Masoud Masasi,Dodoma yetu
KITENDO cha Serikali  kushindwa kulipa deni la bohari ya dawa hapa nchini (MSD) la shilingi bilioni 41 na ufumbuzi wa mgogoro unaondelea wa madaktari ni kati ya sababu, zilizochelewesha kupitishwa kwa bajeti ya wazira ya afya kwenye kamati ya bunge ya huduma za maendeleo ya jamii.

Hayo yalibainishwa mjini hapa jana na mwenyekiti wa kamati ya hiyo Magret Sitta wakati alipokuwa akizindua mtandao wa wadau kuboresha manunuzi ya madawa Tanzania na kufungua warsha ya waangalizi wa taratibu za ununuzi wa madawa.

Sitta  alisema kuwa kamati yetu ilikataa kuipitisha bajeti ya wizara ya afya na kuirudisha Serikalini  kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo bajeti hiyo kutengewa fedha dogo huku ikikabiliwa na madeni, ambapo waliitaka irekebishe baadhi ya maeneo ambayo hawakurishika nayo.

Alisema kwanza kabisa kamati hiyo imeitaka serikali kuhakikisha inalipa deni lote la MSD ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi kwani wamekuwa wakilalamika sana kutokana na deni hilo na kudai kuwa wanashindwa kusambaza dawa hapa nchini kutokana na deni hilo.

Akifafanua kuhusiana na mgogoro wa madaktari alisema baada ya bajeti hiyo kufikishwa mbele ya kamati yao na kubaini kuwa hakuna  maelezo ya kulidhisha kuhusina na mgogoro wa mgomo wa madaktari unaoendelea kufukuta hapoa nchini waliitaka Serikali kutoa maelezo ya kuridhisha na kueleza wamejipangaje kutatua tatizo hilo.

Katika mgogoro huo pia tulitaka kujua wamejiopangaje kuwalipa watumishi wa wizra ya afya wakiwemo madaktari na watumishi wengine ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa moyo mmoja ukizingatia kuwa hiyo ni sekta nyeti ambayo kila mtu anaitegemea na inaathari kubwa endapo itagoma kufanya kazi.

“Tulihoji na kutaka kujua kauli ya Serikali kuhusiana na jinsi ilivyojipanga kumaliza  mgogoro  wa madaktari na watumishi wa wizara ya afya”

Serikali ilitujibu kuwa Waziri mkuu alishaunda tume kwa ajili ya kushughulikia matatizo hayo ambapo nasi tuliwaagiza watuletee taarifa za kazi iliyofanywa na kamati hiyo toka imeundwa ili tuone kma kweli kazi hiyo imeweza kutatua tatizo”Alisema Mwenyekiti huyo.

Alilitaja jambo lingine ambalo lilisababisha bajeti hiyo ya wizara ya afya kurudishwa ni kiasi kidogo cha fedha kilichotengwa kwenye bajeti ya wizara hiyo, suala la upatikanaji wa madawa katika zahanati, hospitali  na vituo vya afya vilivyopo hapa nchini ambalo ni tatizo kubwa.

Alitanabaisha kuwa bajeti hiyo awali Serikali ilitenga shilingi bilioni 62 kwa ajili ya wizara ya afya huku upande wa manunuzi ya madawa pekee walitenga shilingi bilioni 198 , fedha ambazo kidogo sana ukilinganisha na mahitaji na changamoto nyingi zinazoikabili wizara hiyo.

Alisema baada ya kupokea bajeti hiyo kamati ilipiga kelele kwani tangu awali walishakubaliana angalau bajeti ya wizara ya afya ikiwa kidogo basi ifikie asilimia 13 kama sio asilimia 15 lakini cha kushangaza mwaka huu imeshuka hadi kufikia asilimia 9 tu wakati katika bajeti iliyopita ilikuwa asilimia 13.

Alisema baada ya kuibana sana Serikali ilikubali kuongeza shilingi bilioni 5 tu ambazo nazo hazitoshi, na kuongeza kuwa wameaagiza kuchukua pesa kutoka katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukopo ili kuhakikisha wanaongeza katika bajeti ya wizara ya afya.

“Hali hiyo hairidhishi hata kidogo kutokana na umuhimu wa wizara hiyo kwani ukiumwa huwezi kufanya kazi yeyote na wanaotakiwa kutuhudumia ni madktari ambao walipwa kidogo na kufanya migomo”

“ Lakini pia hapa Tanzania tatizo kubwa ni upatikanaji wa dawa kwenye zahanati zetu, vituo vya afya na hospitali lazima tupige kelele” alisma Sitta

Aidha alisema kamati inaendelea kushangazwa na kushindwa kupata majibu kutokana na kulegalega kwa utendaji wa bohari ya dawa licha ya kuanzishwa mika 19 iliyopita ambapo amewaagiza wadau wa mtandao huo uliozinduliwa kuwa karibu na kutafuta ufumbuzi wa tatizo linaloikabili bohari hiyo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa