

Mmoja wa askari wa kikosi cha jeshi la Makutupora cha mjini Dodoma
akifumua tanuri la mkaa lilikuwepo kwenye hifadhi ya Bonde la
Makutupora wakati wa msako wa kuwakamata watu wanaoharibu mazingira
katika vyanzo vya maji ambapo bonde hilo lenye hekta 36,000
limeathiriwa vibaya kutokana na wananchi kuingiza mifugo na shughulii
za ukataji mkaa na kuni.


Afisa Tarafa ya Hombolo katika manispaa ya Dodoma Isaac Songoro
akionyesha sehemu ya miti aina ya mitundulu iliyokamatwa ikikatwa
katika vyanzo vya maji ya Bonde la Makutupora ambalo limeathiriwa na
uharibifu wa mazingira unaofanywa na wananchi wanaishi jirani na bonde
hilo kulia ni afisa uhusiano wa mamlaka ya majitaka na majisafi mjini
Dodoma(DUWASA)Sebastian Warioba juzi mjini hapa.
Picha na Masoud Masasi wa Dodoma yetu
0 comments:
Post a Comment