Mkulima wa zao la Alizeti Eva Sakalani akipukuchua alizeti mara baada
ya kutoka kuvuna shambani kama alivyokutwa katika kijijji cha
Chololo katika Manispaa ya Dodoma,alizeti ni moja ya mazao yanayolimwa
kwa wingi mkoani Dodoma kutokana na kuweza kukabili ukame wa mkoa huu
tofauti na mazao mengine kama mahindi
Mkulima wa mtama aina ya Masia Boniface Chiwanga akiangalia shamba
lake la mtama katika kijiji cha Chololo mkoani Dodoma katika siku
ya mkulima shambani iliyoandaliwa na ofisi ya Manispaa ya Dodoma
kupitia idara yake ya kilimo ambapo mkulima huyo alisema analima mtama
na uwele kwa kuwa unakabiliana na ukame.
Picha na Masoud Masasi wa Dodoma yetu
0 comments:
Post a Comment