Mwandishi Maalumu, Mpwapwa
MKUU wa Wilaya ya Mpwapwa, Christopher Kangoye amesitisha uchimbaji wa madini aina ya ‘copa’ katika Kata ya Lumuma kwa kampuni ya Kimani Minerals Limited kwa madai ya kutofuata taratibu na kuharibu mazingira
Kangoye alisema alifikia hatua hiyo kutokana na mgogoro ulioibuka kati ya
mwekezaji huyo na wanakijiji wa kijiji hicho kwa madai kuwa mwekezaji huyo hajafuata taratibu za uchimbaji wa madini.
Alisema wanakijiji hao wanadai kampuni hiyo inachimba madini kwenye vyanzo vya maji jambo linalohatarisha maisha ya wanakijiji hao.Mkuu wa wilaya alisema alisema kampuni ina leseni ya wachimbaji Wadogo, lakini wanatumia mitambo ya kisasa katika kufanya utafiti wao ambao umejikita katika kuitafuta faida na kuwadhoofisha wachimbaji wadogo na wanakiji kwa ujumla.
Kangoye aliwataka watu wote wanaoishi kwenye vyanzo ya maji vya kijji hicho kuondoka wenyewe kabla hajatumia nguvu za dola kwa ajili ya mstakabali wa Wilaya ya Mpwapwa na vitongoji vyake.
“ Nasema hakuna aliye juu ya sheria, hivyo wito wangu kwa wananchi na wawekezaji wafuate sheria na taratibu ili kuiendeleza Mpwapwa”, alisisitiza.
Alivitaja vijiji ambavyo wakazi wake wanaendesha shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji kuwa ni Lufusi katika Kata ya Lumuma, Kiboriani Mpwapwa mjini na Kwamdyanga katika Kata ya Mpwapwa
mjini.
Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya
Asili ya Tanzania, Laurent Mwakakonyole alidai wawekezaji hao wameingia kwenye misitu ya asili.
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment