Home » » CDA yajipanga kubadili mji wa Dodoma

CDA yajipanga kubadili mji wa Dodoma


Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MAMLAKA ya Ustawishaji ya mji wa Dodoma (CDA), imetenga Sh bilion 16, kwa ajili ya eneo maalumu la uwekezaji ambalo litavutia wawekezaji katika sekta mbalimbali za kiuchumi.

Mradi huo ambao unaitwa Njedengwa Investment Project, unatarajiwa kukamilika baada ya miaka mitatu.

Akizungumza juzi na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa CDA, Mhandisi Paskasi Muragili, alisema, eneo la miundombinu ambazo zitasaidia kupatikana kwa huduma muhimu.

“Eneo hilo litakuwa na barabara za viwango vya lami kwa kilomita 20, katika mradi huo ambao pia utakuwa na huduma mbalimbali za kijamii.”

“Faida za mradi huo ni kuwezesha vijana wengi wa eneo hilo kupata ajira katika sekta za ujenzi, kwani litajengwa viwanda vikubwa na vya kati” alisema.

Aliongeza kuwa, katika kuboresha mipango miji, Dodoma inapaswa kuwa na mabadiliko makubwa kwa kuwa ni makao makuu ya chama na serikali.

Alisema mradi huo wa Njedengwa upo katika eneo la hekta 570, ambazo zitatumika katika kuweka miradi mikubwa.

“Kutakuwa na makazi bora kwa wananchi ambao watajengewa nyumba za kisasa kwa kupata huduma zote muhimu” alisema. 

Kwamba fedha ambazo zitapatikana katika mradi huo zitatumika katika kuanzisha miradi mipya ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu, kwa ajili ya kuwasadia wananchi wenye kipato cha chini.

Kwa upande wa wawekezaji kutoka nje ya nchi alisema watafuata taratibu za kituo cha uwekezaji, ili kupata nafasi ya kuwekeza katika mradi kwa kufuata taratibu na sheria za nchi.
Chanzo: Mtanzania

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa